Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maajabu ya mpaka wa Morocco na Algeria

Muktasari:

  • Miongoni mwa miji ya Morocco ambayo inapakana na Algeria ni Oujda ambao Simba ilifikia na kuweka kambi ya muda kabla ya kucheza fainali na RS Berkane kwenye Uwanja wa Manispaa ya Berkane.

Berkane: MOROCCO na Algeria ni nchi zinazopakana lakini kwa muda mrefu zimekuwa na mgogoro wa kisiasa sababu kubwa ikiwa ni kugombea ardhi baina ya nchi hizo mbili.

Miongoni mwa miji ya Morocco ambayo inapakana na Algeria ni Oujda ambao Simba ilifikia na kuweka kambi ya muda kabla ya kucheza fainali na RS Berkane kwenye Uwanja wa Manispaa ya Berkane.

Katika mji wa Oujda, nchi za Algeria na Morocco zinatenganishwa kwa barabara tu ambapo upande mmoja Algeria ni sehemu ya mji wa Oran na upande mwingine ni wa Morocco uliopo mji wa Oujda.

Hata hivyo wakati nchi hizo mbili zikiwa na mgogoro wa kisiasa, mambo ni tofauti kwa wananchi wao ambao wenyewe wanaonekana kutokuwa na tofauti yoyote na wamekuwa wakishirikiana kwa ukaribu.

Wananchi wa nchi hizo mbili wamekuwa wakivuka upande mmoja kwenda mwingine kufanya manunuzi na kufuata huduma nyinginezo na wenyeji wa hapa wanasema hakujawahi kutokea ugomvi au vurugu baina yao.

Muingiliano baina ya jamii hizo zilizo katika mpaka wa Algeria na Morocco umechangiwa kwa kiasi kikubwa na asili yao ambapo inatajwa kuwa wengi hapo zamani walikuwa jamii moja lakini pia kuweza kuwasiliana kwa lugha za Kifaransa na Kiarabu.

Zipo baadhi ya familia katika mpaka huo ambazo zimetokana na wazazi tofauti kutoka nchi hizo ambapo kuna ambazo baba ni Mualgeria na mama Mmorocco na kuna familia ambazo baba ni Mmorocco na mama Mualgeria.