Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majaliwa avalia njuga maandalizi Chan

Muktasari:

  • Fainali za CHAN 2024 zitafanyika Agosti 2025 katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amezitaka mamlaka zenye dhamana nchini kuharakisha maandalizi ya Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani (Chan) 2024.

Fainali hizo zitafanyika katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda ambazo zitaandaa kwa pamoja Agosti mwaka huu.

Akizungumza katika ziara ya kukagua viwanja vya mazoezi kwa ajili ya fainali hizo, Waziri Mkuu Majaliwa amewaagiza katibu mkuu wizara ya Fedha, na katibu mkuu wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo kwa kushirikiana na katibu mkuu wa Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) kufanya tathmini ya kazi ya ujenzi na ukarabati wa viwanja vya mazoezi vitakavyotumika kwenye michuano hiyo.

Ametoa maelekezo hayo leo baada ya kupokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT, Brigedia Jenerali Petro Ngata ambaye ndiyo wakandarasi wa mradi huo.

“Ndani ya siku tatu hizi fanyeni tathmini mkutane na mkandarasi na tembeleeni stoo na kuhakiki vifaa vyote ambavyo amesema vipo na muwasilishe taarifa kwangu tarehe 1 Aprili 2025,” amesema Majaliwa.

Mkurugenzi huyo alimueleza Waziri Mkuu kuwa kwa ujumla ujenzi na ukarabati umefikia asilimia 80 ya kazi kwa viwanja vyote ambavyo ni pamoja na ujenzi wa sehemu ya kuchezea (pitch) vyumba ya wachezaji (dressing rooms) pamoja na majukwaa.

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu alikagua viwanja vya Gymkhana, Meja Generali Isamuhyo na  Chuo cha Sheria(Law School ) kilichopo Simu 2000 Ubungo.

Michuano ya CHAN 2024 inatarajiwa kufanyika kuanzia Agosti 2 hadi 30 mwaka huu baada ya kuahirishwa mwaka 2024.

Ikiingia kama mwenyeji, Fainali za Chan 2024 zitakuwa za tatu kwa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kushiriki baada ya kufanya hivyo katika fainali za 2009 na 2020 ambazo zote iliishia hatua ya makundi.

Katika fainali za 2009, Tanzania ilishika nafasi ya tatu kwenye kundi lake baada ya kukusanya pointi nne katika mechi tatu ambapo ilianza kwa kufungwa bao

1-0 na Senegal kisha ikapata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ivory Coast na mechi ya mwisho ikatoka sare ya bao 1-1 na Zambia.

Fainali za Chan 2020, Tanzania ilimaliza katika nafasi ya tatu tena ikikusanya pointi nne ambapo ilipoteza dhidi ya Zambia kwa mabao 2-0, kisha ikaifunga

Namibia kwa bao 1-0 na mechi ya mwisho ikatoka sare ya mabao 2-2 na Guinea.