Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbombo anakuja na mabao 20 ya fasta Yanga

New Content Item (1)
Mashine Mpya Yanga hii hapa

Muktasari:

STRAIKA tegemeo wa Nkana ya Zambia, Idris Mbombo amelihakikishia Mwanaspoti kwamba muda wowote anaweza akala mwewe na kutua Jangwani kama viongozi watakubaliana na ofa yake. Mwanaspoti ndilo lilikuwa la kwanza kufichua usajili huo kama ilivyokuwa kwa mkata umeme wa Simba, Taddeo Lwanga.

STRAIKA tegemeo wa Nkana ya Zambia, Idris Mbombo amelihakikishia Mwanaspoti kwamba muda wowote anaweza akala mwewe na kutua Jangwani kama viongozi watakubaliana na ofa yake. Mwanaspoti ndilo lilikuwa la kwanza kufichua usajili huo kama ilivyokuwa kwa mkata umeme wa Simba, Taddeo Lwanga.

Yanga wamekomaa kuhakikisha wanamnasa mchezaji huyo ambaye ni fundi wa kucheka na nyavu kabla dirisha dogo la usajili halijafungwa Januari 15 mwakani.

Hersi Said ambaye ni kigogo wa kamati ya usajili wa Yanga licha ya kutoweka wazi jina la mchezaji huyo alisisitiza; “Tunaleta mchezaji mzuri sana ambaye ataongeza kitu kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga.”

Katika mahojiano na Mwanaspoti ambalo ndilo gazeti pekee alilozungumza nalo tangu aanze dili lake na Yanga; “Kweli nipo kwenye mazungumzo na Yanga kuna bosi wao mkubwa anaitwa Said (Hersi) ndiyo nazungumza naye siwezi kukwambia wanataka kunipa pesa kiasi gani lakini nimewapa ofa yangu nawasubiri waniambie.”

Mbombo anakuja na mabao 20 ya fasta Yanga

“Wakifikia ninapotaka nitakuja haraka hata Januari mapema nitakuwa hapo unajua huyu Said (Hersi) ni mtu mjanja sana ana maneno ambayo kama utakuwa rahisi unaweza kusaini hata bure lakini najua kazi nitakayokuja kuifanya hapo na presha itakayokuwa kwangu.

“Acha kwanza na wao wajipime halafu wakimaliza wataniambia walipofikia kama tukikubaliana vizuri nitakuja kufanya kazi kwa kuwa sasa naona ni wakati muafaka kwangu kuondoka hapa Zambia,”alisema Mbombo ambaye amewahi kucheza Sudan.

Mbombo anakuja na mabao 20 ya fasta Yanga

Mbombo amefichua kwamba mastaa wawili wa Yanga Mukoko Tonombe na Tuisila Kisinda nao wanampigia kumwambia amalize dili hilo haraka na aje kuungana na timu hiyo.

“Naongea nao sana Mukoko na Kisinda lakini Kisinda ni zaidi kila akinipigia ananiuliza nakuja lini,ni winga mzuri sana kama nikimalizana na Yanga nafikiri nitatimiza ndoto za kucheza naye timu moja.

“Tunaongea mengi wananiambia mambo yalivyo mazuri sasa hapo Yanga,nami naona nimekuwa nikiangalia mechi zao kama mbili wana timu nzuri ina viungo wazuri,mimi kama timu ina viungo wazuri na mawinga wazuri kama Kisinda naweza kufunga kuanzia mabao 17 au hata 20,”aliongeza Mbombo ambaye ni Mkongomani huyo anayependelea kuvaa jezi namba 20.