Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkude apata watetezi Yanga

Muktasari:

  • Mkude aliyesajiliwa Yanga msimu uliopita baada ya kumaliza mkataba Simba, amekuwa hana uhakika wa namba, kiasi cha kuonekana kama ameisha, lakini viungo wa zamani wa kimataifa, Nurdin Bakar na Mohammed Banka wamemkingia kifua kwa kusema jamaa boli bado limo ni yeye kuongeza bidii tu.

WAKATI mashabiki wakijiuliza kitu gani kimemkuta kiungo mkabaji mzoefu wa Yanga, Jonas Mkude aliyewahi kuwika kwa karibu miaka 10 mfululizo akiwa na Simba, wachezaji wakongwe waliowahi kukipiga Simba, Yanga na Taifa Stars wameibuka na kumkingia kifua wakisema jamaa bado wamo sana.

Mkude aliyesajiliwa Yanga msimu uliopita baada ya kumaliza mkataba Simba, amekuwa hana uhakika wa namba, kiasi cha kuonekana kama ameisha, lakini viungo wa zamani wa kimataifa, Nurdin Bakar na Mohammed Banka wamemkingia kifua kwa kusema jamaa boli bado limo ni yeye kuongeza bidii tu.

Wakizungumza na Mwanaspoti kwa nyakati tofauti, wakongwe hao walisema bado wanaamini Mkude ana nafasi ya kufanya vitu vikubwa Ligi Kuu, endapo ataamua kuongeza bidii ya mazoezi binafsi, yatakayomshawishi kocha kumpatia nafasi ya kucheza.

Nurdin aliyeitumikia Simba (2004-2007) na Yanga (2007-2013), alisema bado Mkude ni kiungo mzuri anachotakiwa kukifanya ajue kocha anahitaji kitu gani kutoka kwake na akifanyie kazi kwa bidii.

“Mchezaji yoyote asipopata nafasi ya kucheza mara kwa mara anapunguza kujiamini, kwa uzoefu wa Mkude anachotakiwa kukifanya ni uamuzi wa kufanya mazoezi binafsi, yatakayomfanya awe fiti ili kocha akimuona katika mazoezi ya timu amshawishi kumpa mechi,” alisema Nurdin, huku Banka aliongeza; “Japo kwa sasa navutiwa zaidi na uchezaji wa Yusuf Kagoma, bado naamini Mkude ana uwezo mkubwa kinachotakiwa kwake azidishe mazoezi na awekeze zaidi katika kazi, naamini atawashangaza wengi.”

Katika msimu wa kwanza, Mkude aliitumikia Yanga mechi 10 tu akicheza jumla ya dakika 300, tofauti na hali ilivyo msimu huu ambapo amechezeshwa mechi mbili akitumia dakika 26 katika Ligi Kuu na kuzua maneno kwamba ‘jamaa ndio ntolee hivyo’, kwani anaoshindana nao katika eneo la kiungo wamemzidi.

Kwa msimu huu Aucho kacheza mechi 20, dakika 1548, amefunga bao moja katika ushindi wa Yanga wa 5-0 dhidi ya Mashujaa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma wakati Abuya kacheza mechi 22, dakika 1184, kafunga mabao mawili na asisti mbili, jambo linaloendelea kufinya nafasi ya Mkude kupata namba.