Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mpepo atoboa siri za Zesco kwa Yanga

Muktasari:

Were ndiye aliyeibeba ZESCO United ugenini kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Green Mamba kwa kufunga bao pekee lililowafanya  watinge raundi ya kwanza kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-0 kutokana na mchezo wa kwanza  wakiwa kwao Zambia kushinda kwa mabao 2-0.

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Kitanzania, Eliuter Mpepo anayeichezea  Buildcon  ya Zambia,  amewastua  mapema Yanga  wajiandae kuwadhibiti  Were Jesse, Kasumba Umar na Ching’andu John  wa ZESCO United  kwenye mchezo wa  raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga wataanzia nyumbani uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwenye mchezo wa kwanza wa kuwania nafasi ya kuingia makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ZESCO United kati ya Septemba 13 hadi 15.

Mpepo alisema  baada ya kuondoka kwa Lazarous Kambole, Were, Kasumba na  Ching’andu  wamekuwa  wakitegemewa kwenye kikosi cha ZESCO United ambayo inanolewa na kocha wa zamani wa  Yanga, George Lwandamina.

“Mchezaji wao tegemeo msimu uliopita alikuwa Kambole ambaye amejiunga na Kaizer Chiefs, naona kuondoka kwake kumetoa nafasi kwa Were kuwa ndio staa wa timu yao huku wanamwita mfalme.

“Anajua namna ya kuulinda mpira, huwa tunatumia uwanja mmoja wa mazoezi baina ya timu yangu ya Buildcon   na ZESCO kuna siku tuliwahi kufika ilibidi tusubiri wamalize program zao, alikuwa akiwasumbua sana wenzake, ni mwepesi wa uamuzi,” alisema Mpepo.

Mshambuliaji huyo wa Kitanzania aliongeza kwa kusema, Were na Kasumba ni washambuliaji, lakini Ching’andu ni kiungo mchezeshaji mwenye uwezo pia wa kufunga.

Akizungumzia udhaifu wao, Mpepo alisema ZESCO  United wanapitika pembeni kama Yanga watakuwa na mawinga wenye kasi basi ni rahisi kufungika kupitia maeneo hayo.