Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nabi awakingia kifua mabosi Yanga


ALIYEKUWA kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi amewatetea viongozi wa klabu hiyo dhidi ya lawama zinazotolewa kwa kushindwa kusajili wachezaji bora msimu huu.


Nabi amesema kwa uzoefu wake akiwa ndani ya Yanga, viongozi wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kutafuta na kusajili wachezaji wenye ubora, lakini wakati mwingine baadhi yao hushindwa kuthibitisha uwezo waliokuwa nao katika timu walizotoka.

Kocha huyo alisema kabla ya kusajiliwa, wachezaji wengi walionyesha kiwango kizuri katika klabu zao za zamani na walionekana kuwa na sifa zote za kuisaidia Yanga kufikia malengo yake.

“Nimeona watu wengi wakiwalaumu viongozi kuhusu baadhi ya wachezaji waliosajiliwa, lakini ukweli ni kwamba wengi wao walikuwa na viwango bora kwenye timu walizotoka. Walikuwa wachezaji wazuri na walistahili kupewa nafasi,” alisema Nabi ambaye kwa sasa hana timu yoyote anayofundi baada ya kuacha na Kaizer Chief ya Afrika Kusini.

Alieleza kuwa mafanikio ya mchezaji ndani ya klabu hayaamuliwi na viongozi pekee waliomleta, bali yanategemea zaidi nidhamu, kujituma na uwezo wa mchezaji mwenyewe kuthibitisha thamani yake uwanjani.

“Viongozi hawawezi kumsaidia mchezaji ambaye yeye mwenyewe hana nidhamu ya kazi na kujituma. Klabu inaweza kufanya kila kitu kinachowezekana, lakini mwisho wa siku mchezaji ndiye anatakiwa kuonyesha uwezo wake,” alisema Nabi aliyeiongoza Yanga kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara kwanza.

Nabi alisema ana imani kubwa na mfumo wa usajili wa Yanga kutokana na namna viongozi wake wanavyofanya kazi ya kutafuta vipaji na kujadili mahitaji ya timu kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho.

Kwa mujibu wa kocha huyo, vikao vya usajili vya Yanga hufanyika kwa umakini mkubwa na kila mchezaji anayependekezwa hupitiwa kwa kina kabla ya kupewa nafasi ya kujiunga na kikosi hicho.

“Ninaamini Yanga itaendelea kupata wachezaji bora. Nawafahamu viongozi wao na najua jinsi wanavyofanya kazi katika vikao vyao vya usajili. Wana uwezo mkubwa wa kutambua na kuvutia wachezaji wenye ubora,” alisema Nabi.

Kauli ya Nabi inakuja wakati kukiwa na mjadala miongoni mwa mashabiki wa Yanga kuhusu baadhi ya usajili wa misimu tofauti ambao hawakufikia matarajio, huku kocha huyo akisisitiza kuwa jukumu la mafanikio ya mchezaji linabaki mikononi mwake baada ya kupewa nafasi ya kuonyesha uwezo wake ndani ya timu.