Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vita ya Pacome na Fei Toto sio ya kitoto!

PACOME Pict

Muktasari:

  • Licha ya kuikuta timu ikiwa tayari imeanza msimu, Kocha mkuu wa Yanga, Miloud Hamdi alisema Pacome ni mchezaji ambaye anampa vitu vingi uwanjani na amekuwa bora kila eneo anafurahishwa na na kutambua utendaji kazi wake.

YANGA Alhamisi hii itakuwa ugenini ikimkabili Azam FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao viungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Pacome Zouzoua watakuwa na vita yao kwenye kutoa pasi za mwisho.

Kinara ni Fei Toto mwenye pasi 12 zilizozaa mabao na kupachika mabao matano kambani hivyo imemfanya ahusike kwenye mabao 17 kati ya 38 yaliyofungwa na timu yake kwenye mechi 25 walizocheza.

Nyota huyo ambaye msimu uliopita alimaliza nafasi ya pili kwenye ufungaji akiingia kambani mara 19 akiachwa nyuma kwa mabao mawili na kinara Stephane Aziz Ki ambaye alifunga mabao 21 msimu huu ameonyesha ubora kwenye kutoa pasi za mwisho.

Wakati Pacome ambaye kwenye mechi tatu zilizopita ameibuka na tuzo ya nyota wa mchezo mfululizo akihusika kwenye mabao 17 kati ya 62 yaliyofungwa na Yanga ametoa pasi za mwisho tisa na kufunga mabao nane.

Ubora wa Pacome umeongezeka kutokana na kiwango cha kiungo mshambuliaji wa timu hiyo namba zake kuendelea kupanda katika kikosi cha Yanga tofauti na msimu wake wa kwanza.

Pacome msimu huu ametumika kwenye mechi 22 kati ya 24 walizocheza amecheza dakika 1297 akifunga mabao 8 akitoa pasi tisa zilizozaa mabao na kutwaa tuzo sita za mchezaji bora wa mechi.

Zikiwa  zimesalia siku chache kabla ya pambano hilo, gari la kiungo huyo raia wa Ivory Coast limeonekana kuwaka kutokana na kiwango chake na namba zake kuendelea kupanda katika kikosi cha Yanga tofauti na msimu wake wa kwanza.

Ubora wa kiungo huyo msimu huu ambao ni wa pili kwake na wa mwisho kutokana na mkataba aliosaini, ameendelea kuimarika baada ya kupunguza mechi na dakika akifikia rekodi aliyoiweka  Yanga msimu wake wa kwanza.

Pacome alijiunga na Yanga msimu wa 2023/24 akitokea Ligi Kuu ya Ivory Coast alikokuwa mchezaji bora wa msimu (MVP) na alikuja kuongeza nguvu katika eneo la kiungo mshambuliaji akisaidiana na Aziz Ki.

Nyota huyo msimu wake wa kwanza Yanga alipachika mabao saba na asisti nne katika mechi 23 akitumika kwa dakika 1520.

Kwa idadi hiyo ya msimu wa kwanza, Pacome alihusika katika mabao 11 kati ya 71 yaliyofungwa na timu hiyo ikitwaa ubingwa wa tatu kwa kukusanya pointi 80 katika mechi 30.

Msimu huu katika mechi 22 alizocheza akitumika kwa dakika 1297 amevuka rekodi ya kuasisti mara tisa na kufunga mabao nane akivunja rekodi yake mwenyewe ya msimu wake wa kwanza ambao alifunga mabao saba, ikiwa na maana hadi sasa amehusika na mabao 17 ya timu hiyo inayoongoza msimamo ikiwa na pointi 64 baada ya mechi 24.

Licha ya kuikuta timu ikiwa tayari imeanza msimu, Kocha mkuu wa Yanga, Miloud Hamdi alisema Pacome ni mchezaji ambaye anampa vitu vingi uwanjani na amekuwa bora kila eneo anafurahishwa na na kutambua utendaji kazi wake.