Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Penalti ya Pamba Jiji yamshangaza Minziro

MINZIRO Pict

Muktasari:

  • Penalti hiyo ilipatikana baada ya beki wa Fountain Gate kumgonga mguuni James Mwashinga katika harakati za kuokoa juzi, mpigaji Mathew Tegis akagongesha mwamba wa juu na kurudi uwanjani kabla ya kufanya shambulizi lingine lililotoka nje na mchezo kumalizika.

KITENDO cha Pamba Jiji kupewa mkwaju wa penalti dakika ya 90+7 kisha kukosa ilipotoka sare ya 1-1 na Fountain Gate, kimemshangaza zaidi kocha wa timu hiyo, Fredy Felix ‘Minziro’.

Penalti hiyo ilipatikana baada ya beki wa Fountain Gate kumgonga mguuni James Mwashinga katika harakati za kuokoa juzi, mpigaji Mathew Tegis akagongesha mwamba wa juu na kurudi uwanjani kabla ya kufanya shambulizi lingine lililotoka nje na mchezo kumalizika.

Minziro alishangazwa na namna wachezaji wake walivyoonyesha kukataa kupiga mkwaju huo kabla ya Tegis kuchukua jukumu hilo kama alivyofanya dakika ya 22 alipofunga bao la kwanza kwa penalti, lakini ile ya pili bahati haikuwa kwake, akakosa.

‘Vijana wangu kujiamini kumepungua sababu tayari Tegis alishakataa kupiga penalti.. sasa yeyote angeenda kuchukua mpira akapiga.

“Ni kweli tulimuandaa Tegis na penalti ya kwanza alifunga, hii ya pili akakosa kujiamini na bahati mbaya wote wameiogopa kuipiga. Pengine yeyote angepiga vizuri.

“Wapo wapigaji wengi tu kama Mwashinga (James) lakini sijajua kwa nini wameogopa kupiga penalti. Tulishatangaza kwamba mpigaji atakuwa Tegis alipofunga ya kwanza tulitegemea ya pili pia ajiamini akapige lakini akawa mwoga sijajua kwanini,” alisema.

Kwa upande wa Tegisi, aliomba radhi benchi la ufundi na mashabiki wa timu hiyo akiahidi kusawazisha makosa..

Pamba Jiji ilicheza mechi tatu mfululizo nyumbani ikishinda moja dhidi ya Tabora United (1-0) huku mbili ikitoka sare dhidi ya Namungo (1-1) na Fountain Gate (1-1), hivyo kubaki nafasi ya 10 ikifikisha alama 27 katika michezo 26.

Kwa sasa Pamba Jiji ina michezo minne ya kumalizia msimu ambapo miwili itacheza ugenini dhidi ya Simba na KenGold kisha kurudi nyumbani kucheza na KMC na JKT Tanzania.