Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia akutana na Sir Jim Ratcliffe Ikulu Dar es Salaam

KOCHA Pict

Muktasari:

  • Manchester United inashika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England (EPL) ikiwa na pointi 38 katika michezo 31.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Ijumaa, Aprili 11, 2025 amekutana na mmiliki wa Manchester United, Sir Jim Ratcliffe, ikulu, Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, Rais Samia na Ratcliffe wamefanya mazungumzo ya ushirikiano katika masuala ya utalii na michezo.

"Katika mazungumzo yao Rais Samia amemshukuru Sir Jim Ratcliffe kupitia Taasisi yake ya Six Rivers ambayo ina shughulika na masuala ya Uhifadhi, kwa namna inavyofanya vizuri katika kudhibitimuingiliano wa wanyamapori na binadamu kwa kushirikiana na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).    

"Kupitia Taasisi yake ya Six Rivers, Sir Jim Ratcliffeamebainisha kuwa Taasisi hiyo imedhamiria kurejesha hadhiya Hifadhi ya Taifa ya Selous na kuwa na Wanyama wakubwa katika Hifadhi hiyo," imesema taarifa ya Ikulu.

Kukutana huko kwa Ratcliffe na Rais Samia ni kutimia kwa ahadi ambayo bosi huyo wa Man United aliitoa Februari mwaka huu ya kuja nchini pindi alipokutana na katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii, Dk Hassan Abbasi.

Katika mazungumzo hayo ya leo, Ratcliffe amemkabidhi rais Samia, zawadi ya jezi ya Manchester United ambayo imesainiwa na wachezaji wa timu hiyo.

Kwa upande wake Rais Samia, amemkabidhi Ratcliffe zawadi ya picha pamoja na Jezi ya Timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) yenye ujumbe wa, “Amaizing Tanzania”