Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Saadun, awataja Fei Toto, Sillah

SAADUN Pict

Muktasari:

  • Saadun ambaye amekiri kuwa msimu huu ndio bora kwake tangu ameanza kucheza soka kutokana na mafanikio binafsi aliyoyapata kwa kufunga mabao saba na kutengeneza mabao matatu, ameliambia Mwanaspoti kuwa licha ya kushindwa kufikia malengo ya timu, binafsi amefanya vyema

MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Nassor Saadun amesema anaamini kuwa msimu ujao wa soka unaweza kuwa na neema zaidi kwake kuliko huu unaomalizika, huku akiwataja viungo washambuliaji, Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Gibril Sillah kuwa ni sehemu ya mafanikio aliyonayo.

Saadun ambaye amekiri kuwa msimu huu ndio bora kwake tangu ameanza kucheza soka kutokana na mafanikio binafsi aliyoyapata kwa kufunga mabao saba na kutengeneza mabao matatu, ameliambia Mwanaspoti kuwa licha ya kushindwa kufikia malengo ya timu, binafsi amefanya vyema.

Nyota huyo wa zamani wa Geita Gold, Fountain Gate, KMC na MFK Vyskov ya Jamhuri ya Czech, alisema alikuwa na presha kubwa alipokuwa anatua Azam, lakini anashukuru wachezaji wenzake walimuamini na kumpa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kitu ambacho kimetokea.

“Nawashukuru sana Fei Toto, Sillah kwa kuwa sehemu ya mafanikio niliyonayo lakini pia ninakuwa mchoyo wa fadhila nisipowashukuru makocha kwa kuniamini na kunipa nafasi ya kuonyesha nilichonacho msimu huu umekuwa bora sana kwangu,” alisema na kuongeza;

“Malengo yalikuwa kuipambania Azam FC iweze kutwaa taji la ligi lakini mambo yameenda tofauti, sasa tunapambania kuhakikisha tunamaliza katika nafasi ya tatu ambayo pia ni vita dhidi ya Singida Black Stars. Ligi ni ngumu sana na kila mmoja wetu tumekuwa tukihakikisha tunacheza kwenye viwango vyetu,”€  alisema Saadun na kuongeza;

“Natamani kuona ubora niliouonyesha msimu huu unakuwa na muendelezo lengo ni kuongeza namba zaidi, hii ni baada ya kuingia kwenye mfumo wa ushindani kuanzia kwenye kikosi hadi kwenye ligi na hili linawezekana kwa juhudi binafsi na kusikiliza maelekezo ya mwalimu na pia kufanya kazi kwa ushirikiano.”

Saadun akizungumzia msimu kwa ujumla na mechi zilizobaki alisema ni msimu mgumu wenye ushindani, kila timu imevuna ilichopanda na wao wanaendelea kujiweka fiti zaidi ili kumaliza msimu kwa ushindi kwenye mechi zote zilizobaki.

Azam FC imebakiza mechi mbili ikianza na Tabora United nyumbani Juni 18 na kumaliza ugenini dhidi ya Fountain Gate na endapo itapata matokeo kwenye michezo yote miwili itafikisha pointi 63 na kusalia nafasi ya tatu ilipo sasa ikiwa na pointi 57.