Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serengeti Boys mzigoni leo

SERENGETI Pict

Muktasari:

  • Mechi hiyo inatarajiwa kuanza saa 5:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki na kufanyika kwenye Uwanja wa El Bachir mjini Casablanca.

KIKOSI cha Timu ya Taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, Jumatatu hii kitacheza dhidi ya Zambia katika mechi ya kwanza ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U-17).

Mechi hiyo inatarajiwa kuanza saa 5:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki na kufanyika kwenye Uwanja wa El Bachir mjini Casablanca.

Katika michuano hiyo inayofanyika Morocco kuanzia Machi 30 hadi Aprili 19 mwaka huu, Serengeti Boys imepangwa Kundi A ambapo itakabiliana na ushindani mkali kutoka kwa wenyeji Morocco, pamoja na Uganda na Zambia.

Kocha wa Serengeti Boys, Agrey Morris, ameonyesha imani na uwezo wa kikosi chake kufanya vizuri katika kundi hilo na kutinga robo fainali.

“Tuko kwenye kundi gumu, lakini tunaamini tuna kile kinachohitajika ili kufika robo fainali. Hilo ndilo lengo letu kuu kwa sababu linatuhakikishia nafasi ya kucheza Kombe la Dunia,” alisema Morris na kuongeza.

“Watanzania wanapaswa kuwa na imani na wachezaji hawa vijana. Tumejiandaa vyema na kila mmoja yuko tayari kuipigania nchi.”

Katika kuelekea mashindano hayo, Serengeti Boys iliweka kambi nchini Misri huku Morris akisema walikuwa na maandalizi mazuri.

“Kambi ya Misri ilikuwa ya mafanikio makubwa kwetu. Vijana walicheza mechi za kirafiki za kutosha kujiandaa kwa kile tunachotarajia hapa Morocco, ambayo ni kufuzu kwa Kombe la Dunia,” alielezea.