Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba na dakika 90 za kisasi kwa Mlandege Muungano Cup

Muktasari:

  • Timu hizo mbili zitakutana leo saa 2:15 usiku hapa Uwanja wa New Amaan Complex, zikitoka kufuzu siku moja kwenye hatua ya robo fainali Apprili 23, 2026 ambapo mlandege ilitangulia ikiing’oa Singida Black Stars kwa mabao 2-1, kisha usiku huohuo Simba nayo ikakata tiketi yake, ikiitupa nje Mafunzo kwa ushindi wa bao 1-0.

MASHINDANO ya Kombe la Muungano yanaendelea leo utakapopigwa mchezo wa nusu fainali ya pili ikiwakutanisha Mlandege ya Zanzibar dhidi ya Simba itakayoingia na hesabu mbili muhimu kuamua nani atinge fainali kati ya timu hizo mbili.

Timu hizo mbili zitakutana leo saa 2:15 usiku hapa Uwanja wa New Amaan Complex, zikitoka kufuzu siku moja kwenye hatua ya robo fainali Apprili 23, 2026 ambapo mlandege ilitangulia ikiing’oa Singida Black Stars kwa mabao 2-1, kisha usiku huohuo Simba nayo ikakata tiketi yake, ikiitupa nje Mafunzo kwa ushindi wa bao 1-0.

Mlandege ndio timu pekee ya Zanzibar iliyofanikiwa kutinga nusu fainali iki-ziacha Muembe Makumbi City, KVZ na Mafunzo zilizoishia hatua ya robo fainali, ikifanikiwa kulinda heshima kwa Wazanzibar.

Simba ina deni kubwa mbele ya Mlandege ambapo kwenye mechi mbili zilizopita baina ya timu hizo itakumbuka 2023 kwenye Kombe la Mapinduzi iliondoshwa kwa penalti hatua ya nusu fainali baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1 na kwenye fainali Mlandege ikachukua ubingwa ikiichapa Sin-gida kwa mabao 2-1.

Msimu uliofuata wa 2024 mashindano hayohayo ya Mapinduzi, Mlandege ikailiza tena Simba ikishinda kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali likifungwa na Joseph Akondwanao ambaye sasa anaitumikia TRA United.

Matokeo hayo yanaifanya Simba leo kuingia na akili sawasawa ikijua inakwenda kukutana na timu ngumu mbele yao. Simba inataka kuingia kwa hesabu nzuri kwa kupanga kikosi kizito mbele ya wenyeji wao ili kuepuka aibu ya tatu mbele ya wabishi hao wa Zanzibar tofauti na kile ambacho kilicheza mchezo wa nusu fainali ambacho kilikuwa na wachezaji wengi wa timu ya vijana na wengine wasiopata nafasi mechi nyingi za ligi. Hatua ya pili ambayo itaifanya Simba kuutolea macho mchezo huo ni kiu ya mataji ndani ya misimu minne ikibeba Kombe la Muungano pekee mwaka 2024 ambapo itatafuta uwezekano wa kuchukua taji la kwanza msimu huu, kuwatuliza mashabiki wake wakati wakiyatafuta mengine mawili yaliyosalia ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la CRDB.

Juzi Simba ilituliza presha kwa wachezaji wake wakizungukia vivutio vya utalii hapa Zanzibar, ikiwa ni ofa ambayo ilitolewa na Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi, ikiwapa wachezaji wa wekundu hao utulivu kabla ya mazoezi ya mwisho yaliyofanyika jana.

Kocha Steven Barker wa Simba akizungumza kuhusu mchezo huo, alisema amekataa kuiita mechi hiyo kama mchezo wa kisasi lakini akasema ameiandaa timu yake kuwa kwenye hali ya kupata ushindi.

“Sitaki kuichukulia kama ni mechi ya kisasi lakini nadhani kitu muhimu ni kuendelea kutafuta malengo yetu kushinda hii mechi na baada ya hapo twende fainali kutafuta ubingwa,” alisema Barker.

Mlandege ambayo ndio timu iliyoingiza mashabiki wengi kwenye mechi za robo fainali kwa timu za Zanzibar, inataka kulinda hadhi ya Zanzibar ikisema haitaki kuharibu rekodi yao mbele ya Simba.

Timu hiyo itawategemea wachezaji wake wanne ambao ni zao la Azam FC wenye ubora mkubwa wanaoitumikia timu hiyo kwa mkopo wakiwemo beki Vellim Opondo, Mahmoud Haji, fundi wa kupiga pasi Jamal Saleh na washambuliaji wawili waliofunga mabao yaliyowapeleka nusu fainali, Mussa Hassan na Omar Juma.

Kocha wa Mlandege, Hassan Ramadhan alisema kikosi chake kipo tayari kukutana na Simba na kwamba wamejiandaa kwenye kila kitu kuhakikisha wanatinga hatua ya fainali kwa kuwang’oa wekundu hao. “Tumejindaa vizuri kwenda kukutana na Simba, ni timu nzuri na ina wachezaji wazuri, lakini Mlandege tuna hesabu zetu, tunafahamu kwamba hii mechi ni mtoano tumejiandaa kwenye kila kitu ili tushin-de,” alisema Ramadhan.