Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Southampton ya England yamuwinda Miroshi

MIROSHI Pict

Muktasari:

  • Mbali na klabu hiyo, zipo pia nyingine nyingi zilizoonyesha nia ya kumsajili nyota huyo anayemudu kucheza nafasi mbalimbali uwanjani.

INAELEZWA Klabu ya Southampton ya Ligi Kuu England imevutiwa na uwezo wa Mtanzania Novatus Miroshi anayekipiga Goztepe ya Uturuki na imepanga kumsajili dirisha lijalo la usajili Ulaya.

Mbali na klabu hiyo, zipo pia nyingine nyingi zilizoonyesha nia ya kumsajili nyota huyo anayemudu kucheza nafasi mbalimbali uwanjani.

Inaelezwa kuwa Southampton inafikiria kumnunua moja kwa moja Miroshi kama sehemu ya kubadilishana wachezaji na Göztepe kwa ajili ya maadalizi ya msimu ujao.

Klabu hiyo imepeleka majina ya wachezaji wawili wanaowahitaji na mbali na Miroshi yupo pia kiungo Mnigeria Antony Dennis.

Hata hivyo, kuna asilimia kubwa Miroshi kujiunga na timu hiyo kutokana na ushirikiano unaoendelea kwa klabu hizo zinazosimamiwa na kampuni ya uwekezaji michezo, Sport Republic.

Timu hiyo iko mkiani mwa msimamo wa ligi hiyo na kwenye mechi 29 imeshinda mbili, sare tatu na kupoteza 24 na imekusanya pointi tisa.


KWA NINI MIROSHI?

Hili ni moja ya maswali ambayo pengine mashabiki wamekuwa wakijiuliza kwa nini nyota huyo anahusishwa na klabu kubwa Ulaya. Hata hivyo, jibu ni jepesi kutokana na kiwango alichoonyesha kwenye msimu wa kwanza wa Ligi ya Uturuki.

Kwa kiwango alichokionyesha kwenye mechi 19 za Goztepe ni wazi timu hiyo inayopambana kubaki Ligi Kuu England inamtazama kama mchezaji atakayekwenda kuisaidia.

Miroshi tangu ajiunge na Goztepe akitokea Shakthtar Donetsk ya Ukraine ambako alichukua ubingwa wa ligi na kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya amekuwa na kiwango bora.

Kwenye mechi 19 alizocheza kwenye ligi ya Uturuki amefunga mabao manne na asisti moja timu hiyo ikiwa nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi.

Ndiye mchezaji aliyebadilishwa nafasi mbalimbali kwenye timu hiyo, wakati mwingine akicheza kama mlinzi wa pembeni na kiungo na amekuwa akifanya vizuri.