Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania 19 yaifunga Uganda Kriketi

Muktasari:

  • Ari na kujituma katika mazoezi yaliyowachukua miezi mitatu ndiyo kiini cha vijana wa Kitanzania kushinda mchezo huu.

Tanzania imeanza vyema mbio za kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia kwa vijana wa chini ya miaka 19 baada ya kuifunga Uganda kwa mikimbio 73 katika mchezo uliopigwa jijini Lagos, Nigeria siku ya Jumapili.

Ari na kujituma katika mazoezi yaliyowachukua miezi mitatu ndiyo kiini cha vijana wa Kitanzania kushinda mchezo huu.

Tanzania ndiyo walioanza kubeti na kufanikiwa kutengeneza mikimbio 189 wakipoteza wiketi 8 katika mchezo wa mizunguko 50.

Uganda walishindwa kufukuzia alama walizovuna Watanzania baada ya jitihada zao kuishia kwenye mikimbio 116.

Mashujaa wa mchezo walikuwa ni nahodha Laksh Bakrania aliyetengeneza mikimbio 60 kutokana na mipira 111 na Karim Kiseto aliyeleta mikimbio 51 kutokana na mipira  86.

Agustino Meya Mwamele pia alifanya vizuri kwa urushaji baada ya kushinda wiketi  4.

Lakini nyota wa wiketi alikuwa Raymond Francis ambaye peke yake alipata wiketi 5.

Tanzania itacheza mechi yake ya pili na wenyeji Nigeria keshokutwa.