Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Utamu unazidi kunoga huko

Muktasari:

  • Mwanaspoti limefanya utafiti wa pointi zilizokusanywa katika mechi hizo tisa kabla ya jana ambapo Yanga Princess waliwakaribisha Panama FC ya Iringa na Alliance Girls ilikuwa wenyeji wa Tanzanite ya Arusha.

KABLA ya mechi za jana Jumatano za Ligi Kuu za Wanawake Tanzania Bara, unaambiwa klabu zote 12 zilikuwa zimeshacheza mechi tisa na kuzalisha jumla ya pointi 155.

Huu ni msimu wa tatu wa ligi hiyo, tangu ianzishwe chini ya aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Mlandizi Queens ndio walitwaa ubingwa mwaka 2017.

Mwanaspoti limefanya utafiti wa pointi zilizokusanywa katika mechi hizo tisa kabla ya jana ambapo Yanga Princess waliwakaribisha Panama FC ya Iringa na Alliance Girls ilikuwa wenyeji wa Tanzanite ya Arusha.

Mpaka sasa JKT Queens ndio inaongoza kwa pointi 27 wakishinda mechi zote, Kigoma Sisterz ikiwa na pointi 20, imeshinda mechi sita, sare mbili na imepoteza mechi moja.

Wakati Mlandizi Queens mabingwa wa kwanza wa ligi hii wao wamevuna pointi 19 wameshinda mechi sita, sare moja na imefungwa michezo miwili, huku Alliance Girls kabla ya jana Jumatano ilikuwa inamiliki pointi 17 ilikuwa imeshinda mechi tano, sare mbili na imefungwa michezo miwili na Simba Queens ina pointi 16 zilizotokana na kushinda michezo mitano, sare moja imefungwa mechi tatu.

Panama ya Iringa imejikusanyia pointi 16 imeshinda mechi tano, sare moja imepoteza michezo miwili, Yanga Princess wao wanamiliki pointi 12 kwa kushinda mechi nne na kufungwa tano, huku Tanzanite ya Arusha ikiwa na pointi tisa, wameshinda mechi tatu na wamefungwa sita.

Baobab imekusanya pointi tisa imeshinda mechi tatu na kufungwa sita, wakati Marsh Queens ina pointi sita imeshinda mchezo mmoja, imetoka sare tatu na imefungwa mechi tano, Evergreen na Mapinduzi zimetoka sare mbili kila moja na kufungwa mechi saba na kujikuta zikimiliki pointi mbili mbli.

Mbali na pointi ambazo zilikuwa zimekusanywa kabla ya jana Jumatano lakini pia kulikuwa kumepatikana mabao 220 huku JKT Queens ikiwa kinara wa kupachika mabao mengi (61) huku lango lake likigusha mara mbili pekee hivyo ngome yao kuonekana imara zaidi.