Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vita ya kupanda ZPL yapamba moto

Muktasari:

  • Mzunguko wa 21 wa Ligi Daraja la Kwanza Kanda ya Unguja, umeendelea kwa michezo mitatu ambapo Black Sailors imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Sebleni, mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Mao B, Unguja.

SAFARI ya kupambania kukata tiketi ya kushiriki Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) kutokea Unguja, imepamba moto huku vinara wa Ligi Daraja la Kwanza Kanda ya Unguja, Black Sailors wakitoka uwanjani na ushindi.

Mzunguko wa 21 wa Ligi Daraja la Kwanza Kanda ya Unguja, umeendelea kwa michezo mitatu ambapo Black Sailors imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Sebleni, mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Mao B, Unguja.

Wakati Raskazone akiitandika Sharp Boys mabao 2-1 kwenye uwanja wa Tazara, huku Kundemba ikishindi bao 1-0 dhidi ya Urafiki, mechi zote zikichezwa juzi Jumatatu saa 10:15 jioni.

Baada ya ushindi huo, timu zote zimeendelea kusalia kwenye nafasi zake ambapo Black Sailors imefikisha alama 56, Raskazone 52 na Kundemba 38.

Wakati ligi hiyo inasimama kupisha mwezi mtukufu wa Ramadhani, Black Sailors ndiyo ilikuwa ikiongoza msimamo kwa kuwa na alama 53.

Jana Jumanne, ligi hiyo iliendelea kwa kuchezwa michezo miwili ambapo Kikungwi Star ilikutana na Muungano Rangers katika uwanja wa Mao A na Negro United dhidi ya Inter Zanzibar, ikipigwa Dimba la Mao B.

Mzunguko huo wa 21 utamaliza leo Jumatano kwa michezo mitatu, Ujamaa FC itacheza dhidi ya BZL kwenye Uwanja wa Mchangani, ZAFSA dhidi ya Taifa Jang’ombe itachezwa Mao A na New City dhidi ya Paje Star itapigwa Uwanja wa Mao B.

Ikumbukwe kuwa timu zote kabla ya ligi kusimama zilibakisha michezo kumi kukamilisha msimu wa 2025-2026 ambapo timu mbili za juu zitapanda Ligi Kuu Zanzibar na nne kushuka Ligi Daraja la Pili Mkoa.