Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanakimanumanu waanza kujipata

African Pict

Muktasari:

  • Timu hiyo imeshinda michezo miwili mfululizo kwa mara ya kwanza msimu huu, tangu mara ya mwisho ilipochapwa mabao 2-0 na Transit Camp Januari 12, mwaka huu, baada ya kuzifunga Cosmopolitan na Green Warriors kila mmoja wao mabao 2-1.

KOCHA wa African Sports 'Wanakimanumanu', Kessy Abdallah amesema angalau kwa sasa timu hiyo inaendelea kuimarika tofauti na mwanzoni na sababu kuu ni mbili, kuchezea nyumbani na wachezaji kufuata maelekezo yake kwa ufasaha.

Timu hiyo imeshinda michezo miwili mfululizo kwa mara ya kwanza msimu huu, tangu mara ya mwisho ilipochapwa mabao 2-0 na Transit Camp Januari 12, mwaka huu, baada ya kuzifunga Cosmopolitan na Green Warriors kila mmoja wao mabao 2-1.

"Wachezaji wanafuata vyema maelekezo na hata ukiangalia michezo tunayopoteza tulikuwa tunakosa pia bahati tu, nashukuru tunaendelea kuimarika kadri siku zinavyokwenda, hii inaturejeshea morali yetu ya kupambana zaidi mzunguko huu wa pili."

Kessy aliongeza sababu nyingine inayochangia ni sapoti kubwa wanayoipata kutoka kwa mashabiki zao hasa baada ya kuchezea mechi zao za nyumbani Uwanja wa kituo cha TFF Mnyanjani mjini Tanga, tofauti na mwanzoni walipokuwa Jamhuri Morogoro.

Timu hiyo ambayo ni mabingwa wa Kombe la Muungano mwaka 1988, imepanda Ligi ya Championship msimu huu baada ya kushuka daraja msimu wa 2022-2023 iliposhika nafasi ya 14 na pointi 23, huku msimu uliopita ikiwa ndio mabingwa wa First League.