Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanakimanumanu waitana Mkwakwani

TANGA Pict

Muktasari:

  • Ukiachana na Biashara United iliyoshuka daraja baada ya sare ya bao 1-1, dhidi ya Geita Gold, kwa sasa ni timu moja tu inayosubiriwa kuungana nayo moja kwa moja, huku African Sports iliyo nafasi ya 15 na pointi 19, ikihitaji miujiza pekee.

WAKATI African Sports ikiwa katika presha ya kushuka daraja, viongozi na benchi la ufundi wamewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mechi ya mwisho na Transit Camp, itakayopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga, Mei 10.

Ukiachana na Biashara United iliyoshuka daraja baada ya sare ya bao 1-1, dhidi ya Geita Gold, kwa sasa ni timu moja tu inayosubiriwa kuungana nayo moja kwa moja, huku African Sports iliyo nafasi ya 15 na pointi 19, ikihitaji miujiza pekee.

Ikiwa Wanakimanumanu hao itashinda mchezo huo, watajihakikishia nafasi ya kucheza 'Play-Off' kwa kufikisha pointi 22 na ushindi huo utaishusha Transit Camp iliyo nafasi ya 13 na pointi 21, japo ikipoteza itashuka na kuungana moja kwa moja na Biashara.

Mwenyekiti wa kikosi hicho, Ramadhani Sadiki alisema ushindi wa mabao 2-0, walioupata mechi ya mwisho dhidi ya Kiluvya United, umewapa matumaini kushinda mechi ijayo, huku akiwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuwapa sapoti.

Kocha mkuu wa timu hiyo, Kessy Abdallah alisema hesabu zao ni kushinda mechi hiyo ya mwisho, kisha watajipanga tena upya kwa ajili ya 'Play-Off', kwani hawataki kuona kikosi hicho kinashuka daraja moja kwa moja.