Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga rasmi yaachana na Balinya

Muktasari:

Balinya tangu amesajiliwa Yanga amekuwa hana nafasi ya kucheza mara kwa mara katika timu hiyo na mpaka anafikia hatua ya makubaliano ya kuvunja mkataba na timu hiyo

Dar es Salaam. Siku nne kabla ya dirisha dogo la usajili wa Ligi Kuu Tanzania Bara kufunguliwa klabu ya Yanga imetangaza kuachana na mshambuliaji Juma Balinya.

Kupitia idara ya mawasiliano Yanga, walieleza wamefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na aliyekuwa mchezaji wao Balinya kutokea Uganda, ambaye alisajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili kabla ya msimu huu kuanza.

"Yanga tunamshukuru Balinya kwa huduma yake aliyokuwa akitoa alipokuwa akiitumikia klabu yetu lakini tunamtakia kila la heri katika maisha yake ya soka huko aendako kwani tunaimani anaweza kufanya vizuri," alisema idara ya habari na mawasiliano ya timu hiyo.

Balinya tangu amesajiliwa Yanga amekuwa hana nafasi ya kucheza mara kwa mara katika timu hiyo na mpaka anafikia hatua ya makubaliano ya kuvunja mkataba na timu hiyo ameifungia bao moja tu ambalo lilikuwa katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania.

Ikumbukwe Balinya kabla ya kusalijiwa na Yanga wakali wake Mnyarwanda Patrick Gakumba, alikutana na uongozi wa Simba ili kumsajili mchezaji huyo, lakini walishindwana na akaibukia upande wa pili.