Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Straika Mkenya Pamba Jiji apata ahueni

Muktasari:

  • Katika mechi hiyo ambayo kikosi hicho cha ‘TP Lindanda’ au ‘Wana Kawekamo’ kilichapwa bao 1-0, lililofungwa na Mzambia Chanda Chewe, dakika ya 60, Momanyi, alipata majeraha hayo na kukimbizwa Hospitali ya Arusha Rutheran Medical Center.

MSHAMBULIAJI nyota wa Pamba Jiji, Mkenya Mathew Momanyi Tegisi, anaendelea vizuri kwa sasa baada ya kushindwa kuendelea na mechi ya Ligi Kuu dhidi ya timu ya TRA United, iliyopigwa juzi kwenye Uwanja wa Sheikh Amri, Abeid, jijini, Arusha.

Katika mechi hiyo ambayo kikosi hicho cha ‘TP Lindanda’ au ‘Wana Kawekamo’ kilichapwa bao 1-0, lililofungwa na Mzambia Chanda Chewe, dakika ya 60, Momanyi, alipata majeraha hayo na kukimbizwa Hospitali ya Arusha Rutheran Medical Center.

Akizungumza na Mwanaspoti, Daktari wa Pamba Jiji, Frank Grayson, alisema mshambuliaji huyo alipata majeraha ya kawaida tu ya kimchezo yanayotokea uwanjani, ingawa kwa sasa hali yake inaendelea vizuri na tayari ameruhusiwa kutoka hospitali.

“Taarifa zaidi ya chanzo cha tatizo lake tutaitoa baada ya kukamilika kwa baadhi ya vipimo ila kwa sasa itoshe tu kusema anaendelea vizuri na ameruhusiwa kutoka hospitalini, mwanzo ilitushtua sana, lakini kila kitu kiko sawa,” alisema Frank.

Kwa upande wa mshambuliaji huyo alipotafutwa na Mwanaspoti, alisema kwa sasa anaendelea vizuri na anaushukuru uongozi wa timu hiyo, madaktari, benchi la ufundi, mashabiki na wadau wa soka kwa dua zao, baada ya kupata majeraha hayo uwanjani.

Momanyi aliyetokea Shabana ya Kenya, alijiunga na Pamba dirisha dogo la Januari 2025 na hadi mwisho mwa msimu wa 2024-2025, alifunga mabao saba ya Ligi Kuu, akiwa ndiye aliyeongoza katika kikosi hicho cha ‘TP Lindanda’ au ‘Wana Kawekamo’.

Nyota huyo aliendeleza alipoishia akiwa na Shabana FC, kwa sababu kabla ya kujiunga na Pamba alikuwa pia amefunga mabao matano kwao Kenya, nyuma ya mshambuliaji mwingine wa kikosi hicho, Brian Michira, aliyekuwa anaongoza kwa kufunga saba.

Msimu huu wa 2025-2026, tayari nyota huyo amefunga mabao manne ya Ligi Kuu Bara akiwa ndiye anayeongoza ndani ya kikosi hicho, huku bao lake la mwisho, lilikuwa ni la ushindi wa timu hiyo wa bao 1-0, dhidi ya Namungo FC, Februari 10, 2026.