Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Utamu wa Mashemeji Dabi upo hapa!

Muktasari:

  • Hilo huwa ni pambano la pili bora katika soka kwa watani wa jadi Afrika Mashariki baada ya Kariakoo Derby inayohusisha Simba na Yanga.

Mechi ya 99 ya Mashemeji Derby kati ya vigogo wa soka la Kenya, Gor Mahia na AFC Leopards inapigwa leo kwenye Uwanja wa Nyayo jijini  Nairobi ikiwa ni mfululizo wa Ligi Kuu Kenya, msimu huu.

Hilo huwa ni pambano la pili bora katika soka kwa watani wa jadi Afrika Mashariki baada ya Kariakoo Derby inayohusisha Simba na Yanga.

Mechi hiyo inazikutanisha timu hizo zinazofukuzana katika nafasi kwenye msimamo wa ligi, ambapo Gor Mahia inaogoza ikiwa na pointi 56, huku AFC Leopalds ikiwa nazo 55 zote zikiwa zimecheza mechi 28. Kama ilivyo Ligi Kuu Bara zinapokutana Simba na Yanga, mechi ya Mashemeji huibua msisimko wa aina yake kulingana na historia ambapo hubeba uzito wa kiuchumi, kijamii na kimichezo unaovuka mipaka ya uwanja.

HISTORIA INAANDIKWA

Katika historia ya timu hizo tangu zilipoanza kukutana zimefanya hivyo mara 98 kwenye ligi, Gor Mahia ikiongoza kwa ushindi mara 34 dhidi ya 29 wa AFC Leopards, huku mechi 35 zikimalizika kwa sare. Takwimu hizo zinaonyesha jinsi ushindani ulivyo karibu na usio na uhakika, ambapo tofauti ya ushindi kati ya timu hizo mbili ni ndogo kwa miaka zaidi ya miongo mitano ya mvutano baina yao.

Mechi ya leo itakuwa ya 99 inayokuja ikiwa na kumbukumbu nyingine muhimu, kwani Oktoba kumewahi kuwapo dabi nyingi zaidi (21), ikifuatiwa na Aprili (9), jambo linaloifanya mechi ya mwaka huu, 2026, kuwa na uzito wa kipekee wa kihistoria na msimu.

AFC Leopards pia wana rekodi ya kuvutia ya kutofungwa michezo 10 mfululizo kati ya 1998 na 2005, kipindi kinachothibitisha kwamba historia ya dabi hiyo imejaa mizunguko ya ubabe na mabadiliko ya kimbinu.


FOMU YA SASA

Kuelekea mchezo wa leo, timu zote zinaonekana kuwa karibu sawa kwani Gor Mahia imeshinda mechi 17, sare saba, vipigo vinne, huku

AFC Leopards ikishinda mara 16, sare saba, vipigo vitano. Hali hiyo inaongeza msisimko wa mechi hasa baada ya AFC Leopards kushinda  mzunguko wa kwanza wa msimu kwa bao 1-0, Desemba 7, 2025. Ushindi huo umeongeza presha kwa Gor Mahia kulipa kisasi.

Zaidi ya ushindani wa uwanjani, Mashemeji Derby imekuwa chanzo kikubwa cha mapato na mzunguko wa fedha nchini Kenya, kwani makadirio yanaonyesha kuwa mechi moja inaweza kuzalisha zaidi ya Sh150 milioni za Kenya katika uchumi wa siku ya mchezo, huku sekta za usafiri, hoteli, burudani na biashara ndogondogo zikinufaika kwa zaidi ya asilimia 30 ya ongezeko la mapato wakati wa wikiendi ya dabi.

Mwaka jana pekee, mechi hiyo moja ilizalisha takribani Sh7.3 milioni za Kenya katika mapato ya moja kwa moja ya viingilio, huku 2026 ikitarajiwa kuvunja rekodi hiyo kutokana na mvuto wa mchezo na makadirio ya watazamaji zaidi ya 45,000 katika Uwanja wa Nyayo. Mashe meji Derby siyo tukio la ndani tu ya Kenya, bali hufuatiliwa na matangazo katika zaidi ya nchi 15 za Afrika, ikilifanya kuwa moja ya mechi zenye hadhi kubwa zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki, ikibeba taswira ya soka la Kenya kimataifa.