Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bosi Andrea Berta aanza na Nico Williams atue Arsenal

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Staa huyu wa kimataifa wa Hispania, 22, alionyesha kiwango bora akiwa na timu taifa ya Hispania katika michuano ya Euro mwaka jana ambapo taifa hilo lilichukua ubingwa.

MKURUGENZI mpya wa michezo wa Arsenal, Andrea Berta amekutana na wakala wa staa wa Athletic Bilbao, Nico Williams katika siku za karibuni kujadili uwezekano wa kuipata saini yake katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka huu.

Staa huyu wa kimataifa wa Hispania, 22, alionyesha kiwango bora akiwa na timu taifa ya Hispania katika michuano ya Euro mwaka jana ambapo taifa hilo lilichukua ubingwa.

Timu nyingi zilijaribu kutaka kumsajili dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana lakini ilishindikana baada ya fundi huyu kuamua kuendelea kubakia Bilbao.

Msimu huu amecheza mechi 38 za michuano yote na kufunga mabao tisa.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027 na una kipengele kinachomruhusu kuondoka ikiwa timu inayomhitaji italipa Pauni 50 milioni.


Dean Huijsen

LIVERPOOL na Chelsea zipo katika vita ya kuiwania saini ya beki wa Bournemouth mwenye umri wa miaka 19, Dean Huijsen na zinahitaji kumsajili katika dirisha la majira ya kiangazi mwakani. Licha ya kuonyesha nia ya kutaka kumsajili, vigogo hawa watakutana na ushindani kutoka kwa Real Madrid ambayo ipo tayari kutoa Pauni 50 milioni ili kumpata. Beki huyo ameonyesha kiwango kizuri msimu huu akiisaidia timu yake katika Ligi Kuu England.


Assane Diao

MANCHESTER United, Liverpool na Newcastle United zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili winga wa pembeni wa Como na timu ya taifa ya Senegal, Assane Diao, 19, katika dirisha lijalo. Diao ni mmoja kati ya mastaa tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Como na kiwango alichoonyesha tangu msimu uliopita kimesababisha timu nyingi kutaka kumsajili. Man United chini ya Kocha Ruben Amorim inataka kutengeneza timu ya ushindani na inaangalia zaidi wachezaji vijana.


Mohamed Amoura

MSHAMBULIAJI wa Union St-Gilloise ambaye kwa sasa anaichezea kwa mkopo Wolfsburg, Mohamed Amoura yupo katika rada za Arsenal, Liverpool na Nottingham Forest zinazopambana kwa ajili ya kuipata saini yake dirisha lijalo la usajili. Amoura ameonyesha kiwango bora akiwa na Wolfsburg na msimu huu amecheza mechi 27 za michuano yote na kufunga mabao 10.


Sandro Tonali

JUVENTUS inapambana kuhakikisha inamsajili  kiungo wa Newcastle United na timu ya taifa ya Italia, Sandro Tonali, katika dirisha lijalo lakini inataka kupunguziwa bei ya Pauni 70 milioni ambayo timu yake imeiweka ikiwa kuna timu yoyote inahitaji huduma yake. Tonali mwenye umri wa miaka 24, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028. Msimu huu kiungo huyo ameonyesha kiwango bora akiwa na timu hiyo.


Marc Guehi

NEWCASTLE United bado inajipiga kifua kuhakikisha inamsajili beki kisiki wa Crystal Palace na timu ya taifa ya England, Marc Guehi, mwenye umri wa miaka 24, katika dirisha lijalo. Guehi aliingia katika rada za vigogo wengi barani Ulaya baada ya kiwango bora aliachoonyesha akiwa na timu ya taifa ya England katika michuano ya Euro mwaka jana.


Takefusa Kubo

LIVERPOOL wanawasiliana na wawakilishi wa mchezaji wa winga wa Real Sociedad, Takefusa Kubo, mwenye umri wa miaka 23, ambaye amepanga kuondoka Sociedad ikiwa itashindwa kufuzu kucheza michuano ya Ulaya kwa msimu ujao. Mkataba wa Kubo unatarajiwa kumalizika mwaka 2029. Msimu huyu amecheza mechi 43 za michuano yote.


Boubacar Kamara

ASTON Villa ipo katika mchakato wa kumsainisha mkataba mpya kiungo wao wa kimataifa wa Ufaransa, Boubacar Kamara, 25,  ambao utakuwa wa muda mrefu zaidi na lengo ni kuhakikisha anaendelea kusalia katika kikosi chao baada ya vigogo wengi kutaka kumsajili. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.