Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dembele anavyoisaka tena Ballon d’Or kimyakimya

Muktasari:

  • Hata hivyo, nyuma ya mabao matatu ya Dembele kati ya manne iliyofunga Ufaransa kulikuwa na mjadala mwingine uliowahusisha mastaa na wafungaji bora wa ligi tano bora Ufaransa ambao wote bado wapo katika mashindano hayo kina Erling Haaland (Norway na Manchester City), Kylian Mbappe (Ufaransa na Real Madrid), Harry Kane (England na Bayern Munich), Ousmane Dembele (Ufaransa na PSG) na Lautaro Martinez (Argentina na Inter Milan).

BOSTON, MAREKANI: JUZI, ulimwengu wa soka ulishuhudia shangwe la hat-trick ya Ousmane Dembele dhidi ya Norway ambayo inaonyesha kwa nini Ufaransa ni miongoni mwa wapinzani bora wa Kombe la Dunia 2026.

Hata hivyo, nyuma ya mabao matatu ya Dembele kati ya manne iliyofunga Ufaransa kulikuwa na mjadala mwingine uliowahusisha mastaa na wafungaji bora wa ligi tano bora Ufaransa ambao wote bado wapo katika mashindano hayo kina Erling Haaland (Norway na Manchester City), Kylian Mbappe (Ufaransa na Real Madrid), Harry Kane (England na Bayern Munich), Ousmane Dembele (Ufaransa na PSG) na Lautaro Martinez (Argentina na Inter Milan).

Kwa sasa katika jesabu mastaa hao wote wana nafasi ya kubeba tuzo ya Ballon d’Or 2026, lakini namba zinamwangukia zaidia Dembele iwapo atafanikiwa kuvifunika vivuli vya wenzake katika mashindano ya Kombe la Dunia 2026. Hata hivyo, ni bahati mbaya zaidi kwa Mbappe anayecheza naye kikosini Ufaransa kwa sababu hata klabu yake iliambulia patupu katika mashindano ya ndano ya Hispania.

Nafasi anayopewa Dembele ni kubwa zaidi kwa sababu ameiwezesha PSG kubeba ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya 2025/26, Ligi Kuu Ufaransa (Ligue 1), na akikunja lile la Dunia linaloendelea huko Amerika Kaskazini ni dhahiri kwamba hatakuwa na mpinzani kwani atamfunika Mbappe na wenzake.

Na juzi, wakati kila mtu alikuwa akiwatazama nyota wengine, Dembele ndiye aliyelipuka na kugeuka kuwa nyota wa mchezo akivunja kabisa simulizi zote zilizokuwa zikimzunguka Mbappe na kutokuwepo uwanjani kwa Erling Haaland, kwani hat-trick yake katika kombe hili la dunia inaweza kuwa mwanzo wa hadithi ya kweli ya Ufaransa kubeba ubingwa na yeye kuibuka mchezaji bora wa mashindano.

Lakini, kama akikosa, mwingine yupo tayari kuibuka. Hilo halimhusu Dembele na Mbappe pekee, bali pia Michael Olise, Bradley Barcola na Desire Doue, ambaye aliongeza bao la nne katika mchezo huu uliochezwa Foxborough.

Labda Ufaransa, mabingwa wanaotarajiwa wa mashindano hayo wanaonyesha utajiri mkubwa wa vipaji, kama nchi yao inavyojulikana kwa utofauti na wingi wa rasilimali. Hii ni sawa na kuona mshindi wa Ballon d’Or akichukua nafasi ya juu katika mbio za kiatu cha dhahabu, baada ya matumaini ya pambano la moja kati ya Mbappe na Haaland kuvurugwa na mbinu za Norway.

Uamuzi wa kocha Stale Solbakken kuwapumzisha wachezaji wake wote 10 wa kikosi cha kwanza Norway katika kipigo hicho cha mabao 4-1 ulikuwa wa kushangaza, hasa wakati bado walikuwa na nafasi ya kumaliza wa kwanza katika kundi I.

Ingawa kuna thamani ya kuwapa wachezaji wote nafasi ya kucheza Kombe la Dunia, mashabiki wa Norway waliolipa gharama kubwa kusafiri hawakuona walichotarajia, badala yake walikosa pambano la Haaland.

Kwa Dembele kufunga mabao matatu huku Mbappe akishindwa kufunga, alijikuta akipanda juu kwenye orodha ya wafungaji na kusababisha ushindani mkali wa mabao, lakini pia akiliweka jina lake juu katika orodha ya wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mashindano au mfungaji na ama Ballon d’Or kuitetea.

Kutokana na ushindi huo, Ufaransa imekuwa timu ya kwanza tangu Poland 1974 kuwa na wachezaji wawili wanaofikisha mabao manne kila mmoja katika hatua ya makundi, wakilingana na Grzegorz Lato na Andrzej Szarmach. Mashindano hayo pia yamekuwa ya kwanza kuwa na wachezaji watano waliofunga mabao manne au zaidi katika hatua ya makundi (kabla ya mechi za usiku wa kuamkia leo).

Norway sasa inaonekana kuwa na njia rahisi zaidi kwenye droo ya mtoano, ingawa hilo bado lina mjadala. Ufaransa inaweza kukutana na Ujerumani, Uholanzi au Morocco kabla ya nusu fainali na huenda Hispania.

Lakini, Ufaransa haionekani kujali. Walionyesha tena kwamba vipaji vyao vinaweza kushinda changamoto nyingi, hata udhaifu wao wa ulinzi.

Wakiwa na wachezaji kama Dembele, Doue na Barcola wanaoingia kwenye mashindano wakiwa wapya na wenye nguvu, Ufaransa inaonekana kuwa timu hatari zaidi.

Na kama ilivyoonekana, wanaweza kulipuka wakati wowote na hiyo ndiyo inawafanya kuwa tishio kubwa la ubingwa wa Kombe la Dunia.