Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gyokeres ni Arsenal sio Man United

Muktasari:

  • Hata hivyo, kwenye mpango huo hakuna uwezekano wa kwenda kuungana na kocha wake wa zamani wa Sporting CP, Ruben Amorim huko kwenye klabu ya Manchester United kwa sababu haipo kwenye vipaumbele vyake kama hali itabaki kama ilivyo kwa sasa.

LISBON, URENO: STRAIKA wa mabao wa kikosi cha Sporting CP, Viktor Gyokeres yupo tayari kutua kwenye Ligi Kuu England wakati wa dirisha lijalo la usajili ili kwenda kukipiga katika ligi hiyo msimu ujao.

Hata hivyo, kwenye mpango huo hakuna uwezekano wa kwenda kuungana na kocha wake wa zamani wa Sporting CP, Ruben Amorim huko kwenye klabu ya Manchester United kwa sababu haipo kwenye vipaumbele vyake kama hali itabaki kama ilivyo kwa sasa.

Badala yake, kwa mujibu wa ripoti ya A Bola, straika Gyokeres anataka kwenda kujiunga na timu itakayokuwa inacheza mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, hivyo kwenye ishu ya kutua kwenye Ligi Kuu England, timu ambazo kipaumbele chake ni Liverpool, Manchester City na Arsenal.

Mshambuliaji huyo wa kati wa zamani wa Coventry City anadhani sasa yupo kwenye kiwango bora kabisa cha kuachana na Sporting CP na soka la Ureno kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya baada ya kutamba na klabu hiyo ya Lisbon kwa kipindi cha misimu miwili.

Mkataba wake kwenye kikosi cha Sporting CP utafikia ukomo 2028, huku miamba hiyo ya Ureno ikiwa tayari kukaribisha ofa mezani na itakuwa tayari kuzisikiliza kwa ada itakayoanzia Pauni 60 milioni.