Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha: Maguire aanze mbele

Muktasari:

  • Akizungumza na talkSPORT, Redknapp mmoja wa makocha wanaoheshimika nchini England amemshauri kocha wa Man United, Ruben Amorim kutafakari juu ya mshambuliaji wake Rasmus Hojlund ambaye ni mzito na hampi kitu chochote uwanjani.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa zamani wa Tottenham Hotspur, Harry Redknapp amesema angekuwa anaifundisha Manchester United kwa sasa, basi straika wake namba moja angemfanya kuwa Harry Maguire kutokana na namna anavyopambana kuitafutia matokeo mazuri timu hiyo.

Akizungumza na talkSPORT, Redknapp mmoja wa makocha wanaoheshimika nchini England amemshauri kocha wa Man United, Ruben Amorim kutafakari juu ya mshambuliaji wake Rasmus Hojlund ambaye ni mzito na hampi kitu chochote uwanjani.

Ushauri wa kocha huyo umekuja ikiwa ni siku tatu tangu Maguire alipoiwezesha Man United kufuzu nusu fainali ya Europa League kwa bao lake la tano alilofunga kwa kichwa katika dakika ya mwisho ya muda wa nyongeza dhidi ya Olympique Lyon. Man United ilifuzu kwa jumla ya mabao 7-6.

Man United walikuwa nyuma kwa mabao mawili katika muda wa nyongeza, lakini walifunga mabao matatu ya haraka likiwemo la kichwa la Maguire.

Redknapp alisema ushauri wake kwa Amorim unalenga kumfanya amalizie msimu huu akimtegemea Maguire pale mbele kama mshambuliaji namba moja na baada ya hapo ajitafute msimu ujao kwa kusajili washambuliaji.

Kocha huyo anaamini Maguire ambaye alijiunga Man United akitokea Leicester City kwa ada ya Pauni 80 milioni mwaka 2019 anaweza kuwa suluhisho la muda mfupi

Alipoulizwa angekuwa kocha wa Man U angefanya nini kuhakikisha kwamba anamaliza msimu vizuri, Redknapp alijibu: “Unajua ningefanya nini? Ningemchezesha Harry Maguire kama mshambuliaji. Namaanisha kweli. Ana uwezo wa kufunga kwa vichwa, analegwa vizuri. Ningefanya kazi naye huko mbele kwa wiki chache zijazo. (Man U) hawana mtu mwingine. Yule kijana mwingine [Hojlund] hawezi kufunga.”

Aliongeza kuwa, “ningewataka (wachezaji wengine) wampigie mipira mirefu ya juu. Wachezaji wengine wamsogelee. Angefanya kazi kama (Peter) Crouch (straika wa zamani wa Liverpool na Spurs). (Maguire) hana mpinzani hewani. Tumeliona hilo kwa miaka. Maguire anaweza kufanya kazi hiyo kwa muda mfupi.”

Bao la ushindi la Maguire limeweka hai matumaini ya United kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao iwapo itabeba ubingwa wa Europa League licha ya kuwa katika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England kwa sasa.