Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa hawa 13 wapambania maisha

Muktasari:

  • Kwa hali ilivyo kwenye Ligi Kuu England msimu huu, klabu zitakuwa bize sana mwisho wa msimu wakati dirisha la usajili litakapofunguliwa, ambapo kuna mastaa wataingia na kutoka kwenye vikosi vya ligi hiyo.

LONDON, ENGLAND: LIGI Kuu England imebakiza mechi tisa tu huku kukiwa na orodha ya mastaa kibao wanaopambania maisha yao kujua hatima yao kwa msimu ujao.

Kwa hali ilivyo kwenye Ligi Kuu England msimu huu, klabu zitakuwa bize sana mwisho wa msimu wakati dirisha la usajili litakapofunguliwa, ambapo kuna mastaa wataingia na kutoka kwenye vikosi vya ligi hiyo.

Hata Liverpool yenye nafasi kubwa ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu, itakwenda kuwa bize kwenye dirisha lijalo la usajili kunasa mastaa wapya, ukiziweka kando Arsenal, Manchester United, Manchester City, Chelsea na Tottenham Hotspur, ambazo zitalazimika kufanya usajili ili kuboresha vikosi vyao kwa ajili ya msimu ujao.

Kwenye kikosi cha Man United, kocha Ruben Amorim anapambana kupata wachezaji wa kuja kucheza kwa falsafa zake na hilo ndilo linalofanya wachezaji kadhaa wa kikosi hicho kupambana kufahamu hatima ya maisha yao.

Mastaa wanaopambania maisha yao Old Trafford ni pamoja na Joshua Zirkzee, Andre Onana na wakali wawili waliotolewa kwa mkopo, Marcus Rashford na Antony huku Mason Mount, akisumbuliwa na maumivu.

Kwenye kikosi cha Chelsea kuna wakali kama Kiernan Dewsbury-Hall na Christopher Nkunku wanaopambania hatima zao, wakati Arsenal mastaa ambao wanapaswa kupambana kwa sasa kujua hatima yao ya baadaye ni Raheem Sterling, wakati kikosi cha Manchester City ni Kalvin Phillips, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo Ipswich City na Ilkay Gundogan, ambaye anaweza kubadili timu.

Liverpool kocha wao Arne Slot anaweza kufungua milango ya mastaa Wataru Endo, Harvey Elliott na Darwin Nunez, jambo ambalo litawafanya wakali hao kupambania maisha yao.