Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtego! Palace ilivyoushika ubingwa wa Arsenal

Muktasari:

  • Kivipi? Crystal Palace ina mechi mbili dume kweli kweli katika kipindi hiki cha mwisho wa msimu dhidi ya Manchester City, Jumatano ya Mei 13 huku nyingine ikiwa dhidi ya Arsenal, Jumapili ya Mei 24, 2026.

LONDON, ENGLAND: MWISHO wa msimu wa Ligi Kuu England umeingia katika sura nyingine tamu ambayo imeifanya Crystal Palace kujikuta kwenye mazingira magumu huku mbio za ubingwa zikibaki mikononi mwao.

Kivipi? Crystal Palace ina mechi mbili dume kweli kweli katika kipindi hiki cha mwisho wa msimu dhidi ya Manchester City, Jumatano ya Mei 13 huku nyingine ikiwa dhidi ya Arsenal, Jumapili ya Mei 24, 2026.

Kinachonogesha utamu zaidi ni taarifa Palace inaweza kuingiza kitita cha Pauni 10 milioni endapo Arsenal itatwaa ubingwa wa Ligi Kuu England kutokana na kipengele maalumu kilichowekwa katika dili la kumuuza nyota wao wa zamani, Eberechi Eze kwenda Arsenal.

Kwa kawaida, bonusi kama hizi huwa sehemu ya kawaida katika usajili wa wachezaji wakubwa Ulaya, lakini safari hii mazingira yamekuwa tofauti kutokana na ratiba ya mwisho ya ligi.

Arsenal inamaliza msimu kwa kucheza dhidi ya Palace katika mechi inayoweza kuamua ubingwa huku Palace ikijua wazi ushindi wao unaweza kuinyang’anya Arsenal taji na kuwafanya wakose fedha hizo.

Hali hiyo imeibua mjadala mkubwa England kuhusu maadili ya ushindani, presha ya kifedha kwa klabu za kati na namna mpira wa kisasa ulivyoanza kuhusishwa zaidi na biashara kuliko hisia za ushindani wa kawaida.

Kwa sasa Arsenal ndiyo vinara wa msimamo wa Ligi Kuu ya England ikiwa na pointi 79 baada ya kucheza mechi 36 huku Manchester City ikiwa nafasi ya pili na pointi 74 ikiwa imecheza mechi 35.

Hiyo ina maana mbio za ubingwa bado zipo wazi kabisa hasa ukizingatia ratiba ngumu zinazozisubiri timu zote mbili katika siku za mwisho za msimu.

Arsenal itaanza kwa kucheza dhidi ya Burnley kabla ya kwenda kumaliza msimu dhidi ya Palace. Upande wa Man City, wataanza dhidi ya Palace, kisha Bournemouth na mwisho Aston Villa.

Matokeo ya mechi hizo yanaweza kubadili kila kitu katika siku chache. Kitu kinachofanya Palace ionekane ipo kwenye mtego ni ukweli mechi zao zina uwezo wa kuamua bingwa kwa njia mbili tofauti. Kwanza, wanaweza kuizuia Man City kwa kuichukua pointi katika mchezo wao wa katikati ya wiki. Pili, wanaweza kuamua hatma ya Arsenal siku ya mwisho.

Iwapo Palace itashinda dhidi ya Arsenal katika mchezo wa mwisho, inaweza kuipa nafasi Man City kutwaa ubingwa.

Lakini iwapo watapoteza dhidi ya Arsenal, basi inaweza kushuhudia Arsenal ikitwaa taji huku wao wakipata fedha za bonusi kupitia dili la Eze.

Pauni 10 milioni sio mkwanja mdogo kwa klabu kama Crystal Palace, kiasi hicho kinaweza kusaidia usajili wa wachezaji wapya.

MICHUANO YA ULAYA

Ni klabu tatu tu ambazo zinauhakika wa kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hadi sasa huko England ambazo ni Arsenal, Man City na Manchester United, lolote linaweza kutokea kwa timu ambazo zipo nafasi ya nne na ya tano, Liverpool (59) na Aston Villa (59) na wikiendi ijayo watakutana.

Chelsea inaonekana kuwa na mlima mrefu wa kupanda ikiwa nafasi ya tisa na pointi 49 juu yake kuna Brentford (51), Brighton (53) na Bournemouth (55) huku Totenham ikiwa katika vita ya kuwa mbali na hatari ya kushuka daraja vita ambayo wanapigana na West Ham ambayo imetoka kuchapwa na Arsenal katika mechi ya mwisho ya ligi.