Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtoko mpya Arsenal moto

MTOKO Pict

Muktasari:

  • Arteta amepanga kufanya usajili mkubwa kwenye dirisha lijalo ili kuifanya Arsenal kuwa timu tishio baada ya mambo kuwa mabaya kwa kipindi cha karibuni

LONDON, ENGLAND: ARSENAL itakuwa na mwonekano mpya kabisa kwenye kikosi chao cha kwanza msimu ujao endapo kama kocha Mikel Arteta atawapata wachezaji anaowataka dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Arteta amepanga kufanya usajili mkubwa kwenye dirisha lijalo ili kuifanya Arsenal kuwa timu tishio baada ya mambo kuwa mabaya kwa kipindi cha karibuni. 

Imetupwa nje kwenye Kombe la FA katika raundi ya tatu, ikachapwa kwenye nusu gainali ya Kombe la Ligi na Newcastle United na sasa imeachwa pointi 13 na Liverpool kwenye kilele cha msimamo wa Ligi Kuu England.

Arsenal haijashinda taji lolote kubwa kwa miaka mitano sasa, wakati ukame wao kwenye taji la Ligi Kuu England ukiongezeka na kuzidi miaka 20 sasa. Katika kumaliza hilo, Arteta amepanga kufanya kweli kwenye dirisha la usajili likifunguliwa.

Bosi huyo wa Arsenal aliwahi kufanya hivyo huko nyuma, huku kwenye kikosi chake mchezaji ambaye yupo salama kupata namba ni kipa David Raya na ataendelea kubaki golini.

Kipa huyo Mhispania amecheza mechi 15 kati ya 32 bila ya kuruhusu bao kwenye michuano yote msimu huu, hivyo Arteta hana mpango wowote wa kuleta kipa wa kumbadili. Pia, mchezaji mwingine ambaye yupo salama kwenye kikosi ni beki wa kulia, Jurrien Timber. Lakini, kwenye safu hiyo ya ulinzi, Arsenal itawabidi kupambana kwelikweli kuwabakiza William Saliba na Gabriel wasiondoke, ili waendelee kuwa pacha kwenye beki ya kati.

Kwenye beki ya kushoto, kutakuwa na vita kali kati ya Myles Lewis-Skelly na Riccardo Calafiori, lakini kwenye kikosi cha msimu ujao, dogo wa kutokea kwenye akademia yao, atapata nafasi. Declan Rice amekuwa ingini ya Arsenal kwenye sehemu ya kiungo tangu aliponaswa kwa Pauni 100 milioni kutoka West Ham.

Lakini, mchezaji gani atakuja kucheza naye hapo hilo ni swali. Staa wa Real Sociedad, Martin Zubimendi anajiandaa kutua na huenda akaenda kuucheza pamoja na Rice.

Kuwa na uhuru mkubwa wa kusajili nyota wapya, Arteta atahitaji Jorginho na Thomas Partey waondoke mwisho wa msimu. Martin Odegaard ataendelea kupata nafasi kwenye Namba 10, akibaki kuwa nahodha wa timu hiyo licha ya mambo kuwa magumu kwa upande wake msimu huu.

Ukitazama kwenye fowadi ya timu hiyo, kocha Arteta anahitaji kufanya maboresho makubwa. Kinachoripotiwa ni Arsenal itahitaji kumpiga bei mmoja kati ya Leandro Trossard au Gabriel Martinelli dirisha hilo lijalo. Wote wamekuwa na mchango mkubwa kwenye timu, lakini Arteta anataka winga wa kushoto wa viwango vya dunia.

Jambo hilo litawafanya kwenda kumsajili Nico Williams, ambaye alikuwa moto sana na Hispania kwenye Euro 2024. Hata hivyo, kwenye kunasa saini ya winga huyo, Arsenal italazimika kupambana kwelikweli kutokana na timu nyingi kumhitaji.

Kwenye wingi ya kulia, ataendelea kubaki Bukayo Saka, ambaye pengo lake limekuwa bayana tangu akosekane kwenye kikosi kuanzia Desemba mwaka jana. Saka akiwa fiti atarejea moja kwa moja kwenye kikosi na hivyo Ethan Nwaneri ataendelea kutokea benchi.

Kwenye nafasi ya mshambuliaji wa kati, Arsenal itapambana kunasa mtu wa maana katika eneo hilo na kwa sasa kwenye rada yao yupo Alexander Isak wa Newcastle na Benjamin Sesko wa RB Leipzig. Mmoja atanaswa akipige Emirates.

Kikosi cha Arsenal 2025/2026: David Raya; Jurrien Timber, Gabriel, William Saliba, Myles Lewis-Skelly; Declan Rice, Martin Zubimendi, Martin Odegaard; Bukayo Saka, Benjamin Sesko, Nico Williams.