Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Slot: Mchawi wa Federico Chiesa ni Salah

SLOT Pict

Muktasari:

  • Chiesa alianza vibaya katika kikosi cha majogoo hao kutokana na majeraha yaliyochangia asiwe anacheza ama kupewa nafasi.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Liverpool, Arne Slot anaamini sababu mojawapo iliyochangia staa wa timu hiyo, Federico Chiesa kutoonyesha kiwango kilichotarajiwa ni ubora mkubwa unaoendelea kuonyeshwa na Mohamed Salah kwa msimu huu.

Tangu ajiunge na Liverpool katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana, Chiesa amecheza dakika 387 tu za michuano yote.

Chiesa alianza vibaya katika kikosi cha majogoo hao kutokana na majeraha yaliyochangia asiwe anacheza ama kupewa nafasi.

Mchezaji huyu wa kimataifa wa Italia alionyesha kiwango bora katika mchezo wa fainali ya Carabao Cup dhidi ya Newcastle akifunga bao la jiooni ambalo bado halikuisaidia Liverpool.

Hata hivyo, Slot amesisitiza kwamba bado anamwamini staa huyu licha ya kwamba msimu huu amecheza dakika 25 tu katika Ligi Kuu England.

"Kwa sasa, anashindana na Mo Salah na sidhani kama unaweza kusema Mo ana msimu mzuri, hii imekuwa ni kawaida yake. Hiyo inamfanya (Chiesa) kuwa na changamoto lakini tunajua tunaweza kumwamini pale tunapomhitaji. Sio yeye tu bali hata wachezaji wengine ambao hawapati nafasi, tutawategemea na kuwachezesha pale tunapowahitaji.

"Chiesa ilikuwa vizuri kuona alivyoshiriki kwenye mchezo (dhidi ya Newcastle) alipoingia. Hiyo imekuwa ikitokea mara nyingi msimu huu pale wachezaji walipoingia walifanya tofauti na kubadilisha kabisa michezo, Harvey Elliott naye amefanya hivyo katika mechi tatu au nne za hivi karibuni. Ni sehemu ya kazi yangu na kazi ya mchezaji kuwa tayari kwa wakati tunapomhitaji."