Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

'Come Back' ya Jay Melody si ya kitoto!

JAY Pict

Muktasari:

  • Hata hivyo, Jay Melody alishapotea kabisa katika ramani ya muziki Bongo ila akafanikiwa kurejea tena kwa kishindo cha aina yake na kuutawala mchezo kwa asilimia kubwa kuliko ilivyokuwa hapo awali.

MIONGONI mwa wasanii wa Bongo Fleva wanaofanya vizuri kwa sasa ni pamoja na Jay Melody ambaye nyimbo zake zimekuwa maarufu sana hasa upande wa kinadada huku zikijizolea mamilioni ya wasikilizaji katika majukwaa ya kidijitali.

Hata hivyo, Jay Melody alishapotea kabisa katika ramani ya muziki Bongo ila akafanikiwa kurejea tena kwa kishindo cha aina yake na kuutawala mchezo kwa asilimia kubwa kuliko ilivyokuwa hapo awali.

Mwanamuziki huyu aliwahi kunolewa pale Tanzania House of Talent (THT) alipotoka na wimbo wake, Goroka (2018). Zilifuata nyingine mbili zilizofanya vizuri ambazo ni Namwaga Mboga (2018) akiwa na Nandy, na Mikogo Sio (2018) akiwa na Dogo Janja.

Ila baada ya hapo nyimbo alizotoa hazikufanya vizuri, hali ilikuwa mbaya zaidi kufuatia kifo cha Ruge Mutahaba mwaka 2019 ambaye alikuwa ni mwalimu na msimamizi wake kimuziki pale THT na mtu aliyempa jina hilo la Jay Melody ambalo sasa ni chapa kubwa.

Kufuatia kifo cha Ruge, mashabiki wengi waliamini hatoweza kuja kuwika tena kimuziki, na ni kweli alipotea, mfano nyimbo zake tatu za mwanzo video zake zilitazamwa zaidi mara milioni 1 YouTube ila baada ya hapo hakuweza kufikia tena namba hizo.

Jay Melody katika moja ya mahojiano yake alikiri hali ilikuwa mbaya kwake kimuziki hadi kufikia hatua ya kwenda kwa mganga na kuishi kabisa huko ili kutazama nyota yake na kujua kwanini hafanyi vizuri kama alivyoanza. 

Licha ya yote bado aliamua kujaribu tena, hakukata tamaa, bado aliiona nafasi yake katika Bongo Fleva, aliamua kuwa na moyo wa ujasiri na sasa anavuna matunda ya hatua hiyo muhimu aliyochukua.

Januari 2021 aliachia wimbo wake 'Huba Hulu' ambao ulikuwa mkubwa kila kona, kuna mashabiki ambao ndio walimjua Jay Melody kwa mara ya kwanza kupitia wimbo huo uliofanya vizuri kuliko zile za mwanzo (Goroka na Namwaga Mboga) ambazo zilimtambulisha.

Baada ya kutamba na Huba Hulu (2021), Jay Melody aliachia nyimbo nyingine kama Najiweka (2021) na Sugar (2022) ambao hadi sasa video yake imetazamwa zaidi ya mara milioni 18 YouTube, huku ukimpatia Sh30 milioni kutokana na show ndani ya miezi mitatu tu!.

Kubwa zaidi ni wimbo wake, Nakupenda (2022) uliofunika mitaa yote, ndio wimbo pekee wa Bongo Fleva uliofanya vizuri zaidi katika majukwaa yote ya kidigitali ya kusikiliza muziki kwa mwaka 2022 na hadi sasa unaongoza kwa baadhi ya majukwaa. 

Mathalani ndio wimbo wa Bongo Fleva uliosikilizwa zaidi (most streamed) Boomplay Music kwa muda wote ukiwa umesikilizwa zaidi ya mara milioni 85.7, na kuanzia hapa kila kitu kilibadilika kwa Jay Melody na mengine sasa ni historia.

Kutokana na mapokezi hayo, Jay Melody aliweka rekodi kama msanii wa kwanza Afrika Mashariki kwa kusikilizwa zaidi ya mara milioni 200 Boomplay bila kuwa na albamu wala EP na sasa anashika nafasi ya tano Bongo kwa kufanya vizuri katika jukwaa hilo.

Vilevile wimbo wake 'Nakupenda' ulishinda Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) 2022 kama Wimbo Bora wa Mwaka ukizibwaga nyimbo nyingine kali kama Pita Huku (Dulla Makabila), Nitaubeba (Harmonize), Kwikwi (Zuchu) na Mwamba (Rayvanny).

Na msimu huo, ndipo Billnass alishinda tuzo yake ya kwanza ya TMA baada ya kutoa wimbo wake, Puuh (2022) akimshirikisha Jay Melody ambao ulimuwezesha kushinda kipengele cha Msanii Bora wa Kiume wa Hip Hop 2022.

Utakumbuka Jay Melody ni msanii wa 13 Tanzania kufikisha wafuasi (subscribers) zaidi ya milioni 1 YouTube akiwa ni mmoja ya wasanii wachache waliofika namba hizo ndani ya muda mfupi akiwa amejiunga na mtandao huo Desemba 9, 2017.

Waliomtangulia ni Diamond Platnumz, Rayvanny, Mbosso, Zuchu, Alikiba, Lava Lava, Nandy, Marioo, Aslay, Rose Muhando na Jux, mshindi wa tuzo za Trace 2025 mwenye albamu mbili, The Love Album (2019) na King of Hearts (2022).

Albamu ya kwanza kutoka kwa Jay Melody, Therapy (2024) yenye nyimbo 12, ni miongoni mwa albamu zilizofanya vizuri Bongo mwaka uliopita ikitoa nyimbo maarufu kama Wa Peke Yangu, Siyawezi, 18, Forever n.k.

Kwa sasa Jay Melody ni kati ya wanamuziki wanaoshirikishwa zaidi, miongoni mwa waliomshirikisha ni Diamond (Mapoz), Alikiba (Hatari), Rayvanny (Slow), Phina (Manu), Jux (I Need You), Barnaba (Only You), Mabantu (Fala) n.k.

Pia ameshiriki kuandika nyimbo za wasanii wengi, mfano ndiye msanii aliyemwandikia Nandy nyimbo nyingi zaidi na zote zikafanya vizuri, nyimbo hizo ni Kivuruge (2017), Njiwa (2018), Hallelujah (2019) na Do Me (2020).

Kipindi amepotea kimuziki aliwahi kulalamika kuwa alimsaidia sana Nandy lakini mwenzake alipofanikiwa alimsahau ila sasa meza imepinduka kwani Jay Meledy anakimbiza sana kwenye majukwaa mbalimbali ya kusikiliza muziki kuliko hata Nandy.

Pengine hilo ndilo lilimsukama Nandy kuona sababu ya kumaliza tofauti zao zilizojitokea, Nandy alisema huwenda mwaka huu kolabo yao ikatoka, hilo haliji kwa bahati mbaya bali uwezo na ushawishi alionao Jay Melody kimuziki ukanda huu wa Afrika Mashariki.