Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aslay achefukwa na ishu za mitandaoni

ASLAY Pict

Muktasari:

  • Amepiga stori na Mwanaspoti alisema, watu wa mitandaoni wapo kutumia nguvu ya kusapoti vitu ambavyo havina msingi na kuacha kusapoti kazi ya msanii au biashara ya mtu.

MWIMBAJIi Aslay amewaumbua baadhi ya mashabiki wa mitandao ya kijamii akisema asilimia 99 wanaitumia mitandao hiyo vibaya.

Amepiga stori na Mwanaspoti alisema, watu wa mitandaoni wapo kutumia nguvu ya kusapoti vitu ambavyo havina msingi na kuacha kusapoti kazi ya msanii au biashara ya mtu.

"Yaani Tanzania ndio nchi ambayo tunaweza sema inawatu wanaopenda kusapoti vitu vya ovyo kuliko vya maana huko mitandaoni, yaani utakuta wakianza kushabikia kitu cha msanii ama mtu maarufu yeyote kwa kuzungumzia vibaya  tovuti na huyo mtu akifanya kitu kizuri au kutoa nyimbo wanakupoteza kabisa na  kuanza kukujadili ,hii ni figisu ambayo mbaya sana kwa watumia mitandao ya kijamii

"Tena wapo radhi kukutungia habari za uongo na kuzitrendisha huko mitandaoni hasa pale wakiona umetoa wimbo wako au Albam yako, au umefanya kitu cha msingi kama ni mtu mashuhuri, ndio wanataka kukuharibia ili kazi yako isiende mjini, wapo wenyewe wa kujiita wazee wa kufukua makaburi yaani mambo ya zamani za kale wanayaleta kwa sasa ilimradi tu kukuondoa kwenye trending ya tukio lako ambalo wanalitia figisufigisu tu" alisema Aslay

Alisema imefika wakati watu waache tabia ya kupenda kuongelea habari za watu kuliko kazi zao ama mambo yao ya msingi.

"Watu wanatakiwa kuondokana na ujinga walionao wa kusapoti ujinga na kuacha kusapoti vitu vya maana vya mtu, kiufupi waache umbea umbea, yaani huu umbea wanaoufanya ungekuwa ndio wanapush kazi zetu basi Tanzania tungekuwa mbali kimuziki," alisema.