Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

PUMZI YA MOTO: Yanga, Simba zisitufanye tuidharau busara

PUMZI Pict

Muktasari:

  • Namna ambayo BUSARA inavyozungumzwa kwenye mijadala yao, utadhani ni kitu fulani hivi kibaya na cha hovyo ambacho hakifai kabisa kutumika.

"Mpira wetu unaharibiwa na TFF kwa sababu wanatumia BUSARA badala ya kanuni."

Maneno haya si mageni hapa jijini, hasa baada ya mechi ya watani wa jadi, Yanga na Simba, kuota mbawa.

Mashabiki mitaani, wanaojiita wachambuzi wa soka, na hata wanasiasa, lawama zao ni kwa Bodi ya Ligi na TFF kwa kutumia busara kufanya maamuzi na siyo kanuni.

Maamuzi hayo ni kuahirisha mechi ya watani wa jadi kutoka Machi 8 hadi itakapotangazwa tena.

Namna ambayo BUSARA inavyozungumzwa kwenye mijadala yao, utadhani ni kitu fulani hivi kibaya na cha hovyo ambacho hakifai kabisa kutumika.

Hapa ndipo panaponitia shaka. Ina maana vichwa vya Watanzania vimevurugwa na Yanga na Simba kiasi kwamba BUSARA kwao kinakuwa kitu cha hovyo?

Ina maana jamii ya kitanzania imefikia hatua haitaki tena BUSARA?

Sitaki kuamini hivyo.

PUM 01

MAANA YA BUSARA

Busara ni wito unaofanya akili izingatie kwa makini hali halisi ili kutambua yaliyo mema na kuchagua njia ya kufaa kuyafikia.

Wito huu hauchanganyikani na woga unaomzuia mtu kutenda inavyotakiwa.

Wito huu pia hauchanganyikani na ghilba,  wala ujanja unaotumia hadaa na ulaghai.

Kwa kifupi, BUSARA ndiyo kanuni kuu...kanuni nyoofu ya utendaji.

Popote panapotumika busara ni lazima mambo yataenda vizuri.

Ukiona sehemu mambo yameharibika halafu watu wanasema ni kwa sababu ya busara, kataa...hao ni waongo.

Busara haiharibu mambo, busara inafanya mambo yatulie.

Maamuzi ya Bodi ya Ligi na TFF kuiahirisha mechi ya watani wa jadi yalikuwa yenye busara kuu na wanatakiwa kupongezwa badala ya kubezwa na kutwezwa.

Kusimamia mpira ni jambo gumu sana kwa sababu watu unaowasimamia wanaongozwa na hisia na mihemko halafu wewe msimamizi huna nguvu ya dola kupambana na hisia na mihemko yao.

Moja ya nguvu chache ambazo wasimamizi wa mpira wanayo duniani kote ni kupanga na kupangua mechi.

Hii ni nguvu kuu isiyo na kipimo ambayo ipo mikononi mwao.

Wao ndio watapanga tarehe na muda wa mechi, na hawalazimiki kutoa sababu ya kupanga kwao.

Na wao ndio watapangua terehe na muda wa mechi, bila kulazimika kutoa sababu ya kupangua kwao.

Haya ni mamlaka yanayoanzia kwa FIFA kama chombo kidunia, CAF kama chombo cha kibara, na TFF kama chombo cha kitaifa.

Mechi hupangiwa tarehe na muda kwa mujibu wa kanuni, na hupanguliwa tarehe na muda kwa mujibu wa kanuni.

Na kanuni zote huishia na kifungu hiki cha maneno, 'Sababu zitakazokubalika kwa...aidha FIFA, au CAF au TFF.

Wao ndio wana vigezo vyote vya mechi kuchezwa au kutochezwa.

Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports mwaka 2024 lilipangwa kufanyika Karatu, lakini kwa sababu zilizokubalika kwa TFF, ikapelekwa Zanzibar.

Fainali za CHAN 2025 zilipangwa kufanyika Februari 2025, lakini kwa sababu zilizokubalika kwa CAF, sasa zitafanyika Agosti.

Fainali za Kombe la Dunia 2018 zilipangwa kufanyika Juni - Julai, lakini kwa sababu zilizokubalika kwa FIFA,  zikapelekwa Novemba- Disemba

Haya ni mamlaka waliyojipa wasimamizi wa mpira...dunia nzima.

PUM 02

KWANINI?

Nimesema hapo juu kwamba mamlaka za usimamizi wa mpira zina uwezo wa kupanga na kupangua tarehe na muda wa mechi bila kulazimika kutoa sababu.

Wakitoa, sawa...lakini hata wasipotoa sawa. Wanakuwa hawajavunja kanuni yoyote

Hii ni kwa sababu siyo kila kitu kinapaswa kuwekwa wazi.

Hebu dhania, mechi imepangwa kufanyika leo jioni, lakini mchana watu wa usalama wa raia wakapata taarifa za kiintelijensia kwamba kuna magaidi wamepanga kulipua mabomu uwanjani.

Wakawaambia TFF kwamba mechi isichezwe...na TFF wakaiahirisha...unataka watoke na kusema sababu...si wataingilia uchunguzi na hao magaidi kujificha zaidi?

Ndio maana mamlaka za mpira hazilazimiki kutoa sababu ya kupanga au kupangua mechi yoyote...wakitoa sababu sawa, wasipotoa napo ni sawa tu...ilimradi sababu hizo zimekubalika kwao.

Wao ndio wanatakiwa kuzipima sababu na kufikia maamuzi. Kwenye kufanya hivyo, lazima waongozwe na BUSARA.

Kwa sababu BUSARA ndiyo kanuni kuu...kanuni nyoofu ya utendaji.

Kwa sababu BUSARA ni wito unaofanya akili izingatie kwa makini hali halisi ili kutambua yaliyo mema na kuchagua njia ya kufaa kuyafikia.

PUM 03

KUKOSA BUSARA

Mechi ya Yanga na Simba haikufanyika sio kwa sababu Bodi ya Ligi na TFF wakitumia BUSARA, hapana.

Haikufanyika kwa sababu kuna watu walikosa busara na weledi na kusababisha mikanganyiko.


I. Kamisaa kukosa weledi

Jioni ya Machi 7 Simba kama wageni, walienda Uwanja wa Mkapa kufanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo wao wa Machi 8.

Inasemekana hawakutoa taarifa kwa Kamisaa wa mchezo kwamba wangeenda, hivyo Meneja wa uwanja akashindwa kuwafungulia kwa sababu hakuwa na taarifa kama watakuja.

Hii ni moja ya mambo ya kitoto sana kwa sababu haya mambo hupaswa kujadiliwa kwenye mkutano wa kiufundi kabla ya mchezo (pre match meeting) ambao kamisaa wa mechi huwa mwenyekiti.

Kwa hiyo kamisaa yeye ndiyo alipaswa kulifanya hilo kama moja ya ajenda za mkutano ule, kama hakufanyika basi kosa ni lake yeye kama msimamizi mkuu ya mechi hiyo.

Na kuonesha kwamba hii haikuwa shida ya Simba, wakaruhusiwa kuingia.


II. Yanga na mabaunsa kukosa busara

Watu wanaoitwa 'mabaunsa' wa Yanga wawazuia Simba kuingia uwanjani baada ha meneja wa uwanja kuwafungulia Simba.

Huku ni kukosa busara kwa mabaunsa hao na waliowatuma.

Ile ni siku ya mazoezi ya Simba, Yanga hawakupaswa kabisa kuwepo pale...uwepo wao ni kutokana na kukosa kwao busara tu.

PUM 04

III. Simba kukosa busara

Simba nao walipokataliwa kuingia wakasusa na kurudi kwao kulala...halafu wakatoa tamko la kugomea mechi.

Huku ni kukosa busara kwa kiwango kikubwa sana na walionesha ni kwa namna gani busara yao iko chini.

Busara ni wito unaofanya akili izingatie kwa makini hali halisi ili kutambua yaliyo mema na kuchagua njia ya kufaa kuyafikia.

Simba walipaswa wazingatie kwa makini hali halisi na kutambua yaliyo mema na kuchagua njia ya kufaa kuyafikia.

Walitakiwa watambue umuhimu wa mchezo hivyo wafanye kila linalowezekana ili wafanye mazoezi na kesho wakacheze mechi.

Lakini kwa kukosa kwao busara, wakasusa.

Yaani ni sawa na mtoto asiyependa kwenda shule, kaamka asubuhi hajauona mswaki wake, kasusa kwenda shule...kukosa busara.


IV. Yanga kukosa busara na kwenda uwanjani

Bodi ya Ligi ilitoa taarifa rasmi saa saba mchana kwamba mechi imeahirishwa. Lakini Yanga kwa kukosa kwao busara wakaenda uwanjani.

Walienda kufanya nini kama sio kutafuta shari na kutengeneza taharuki?

Ingetokea fujo pale uwanjani, nani angewajibika?

Hii ni klabu inayoongozwa na Rais wa Klabu barani Afrika, inashindwaje kujielewa namna hii?


V. Yanga kukosa busara na kudai alama tatu

Baada ya kwenda uwanjani, Yanga wakaandika barua TFF kudai alama tatu kutokana na Simba kutofika uwanjani.

Hii ni ishara nyingine ya Yanga kukosa busara kwa kiwango kikubwa sana.

Hivi kweli Yanga hawajui taratibu za mchezo?

Ili timu ambayo haikufika uwanjani ihesabiwe imepoteza mchezo na iliyofika kupewa alama tatu za mezani, ni lazima taratibu zote za mchezo zifanyike.

Kuwe na waamuzi, timu iliyofika ikaguliwe na iingie kiwanjani.

Mwamuzi asubiri dakika 30 kisha apige filimbi ya kumaliza mchezo.

Hapo ndipo timu iliyofika inastahili kupata alama tatu.

Lakini ule mchezo uliahirishwa na japo wao walienda uwanjani, hakuna taratibu zozote za mchezo zilizofanyika...unadai vipi alama tatu?

Hii inatoa picha halisi ya klabu hii kongwe inavyoendeshwa kihuni...na ndio maana hawajawahi kushinda kesi kila wanaposhitaki au kushitakiwa. Kwa sababu wanakosa busara.

Tusifikie hatua tukadharau matumizi ya BUSARA kwa sababu za mihemko ya mpira.

Busara haijawahi kuwa kitu kibaya. Busara haijawahi kutoa matokeo mabaya.

Ni kukosa busara ndiyo husababisha mitafaruku.