Barnaba hapigi mke kwa ngumi
Muktasari:
- Hivi karibuni kumeibuka stori hizo na Barbana imedaiwa kuwa na tabia hiyo hadi mke wake kuondoka mara kwa mara na kurudi nyumbani kwao.
BAADA ya kuzuka kwa stori msanii wa Bongo Fleva, Elias Barnabas 'Barnaba Boy' amekuwa akimpiga mkewe, mkali huyo ameibuka na kujibu, hana muda huo na haijawahi kutokea.
Hivi karibuni kumeibuka stori hizo na Barbana imedaiwa kuwa na tabia hiyo hadi mke wake kuondoka mara kwa mara na kurudi nyumbani kwao.
Hata hivyo amefunguka alipohojiwa na Mwanaspoti akidai yeye sio aina ya wanaume wanaopiga wake zao kwa ngumi, ila hupiga kwa kutumia maneno zaidi.
Barnaba amesema hajawahi kumpiga mkewe hata kofi kama watu wanavyosema, bali anatumia maneno kumrekebisha.
“Si jambo zuri kumpiga mwanamke na katika maisha yangu, sijawahi kumpiga mwanamke, ila maneno yangu yanatosha kumchapa," amesema Barnaba.
Ishu ya wanaume kuwapiga wapenzi wao imekuwa 'hot' hivi karibuni, hata hivyo, staa huyo wa ngoma kama Lover Boy, Zodoa, Wahalade, Sichomoi, Nibusu na Chausiku alisisitiza hana muda wa kumpiga mwanamke ngumi, kwani anajua mke anapigwa na upande wa khanga au kumuonya tu kwa maneno.