Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dulla Makabila, Barnaba kuwasha moto tamasha la Sauti za Busara

Muktasari:

Tamasha la Sauti za Busara hii ni mara yake ya 18 kufanyika ambapo wasanii mbalimbali wamekuwa wakialikwa kutoka nchi za bara la Afrika.

Wasanii Dulla Makabila na Barnaba Classic wanatarajiwa kuwa moja ya wasanii watakaowasha moto katika tamasha la sauti za  Busara litakalofanyika visiwani Zanzibar mwezi Februari .

Hayo yamebainika leo Jumatano Januari 20, 2021 katika mkutano wa waandishi wa habari na waratibu wa tamasha hilo, uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Yusuf Mahmoud amesema jumla ya vikundi saba kutoka nje ya nchi na saba wa ndani ya nchi watashiriki wakiwemo wasanii Barnaba na Dulla Makabila.

Akielezea sababu ya kumchukua Dulla, Mahmoud alisema ni kutokana na kuimba muziki wenye vionjo vya Afrika ambapo ni moja ya sifa ya msanii kuweza kushiriki katika tamasha hilo.

"Mwaka jana tuliona pia msanii wa singeli Skedu alifanya vizuri tulipomualika kwenye tamasha hili na watu walionekana kumpenda, hivyo na mwaka huu tukaona tusimuache msanii wa singeli na tukamchagua Dulla kwani naye anafanya vizuri kwenye muziki huo na siku hiyo atauimba live," amesema Mahmoud

Hata hivyo amesema tamasha hili kwa mwaka huu likiwa mara yake ya 18 kufanyika lina kauli mbiu ya 'Mazingira Yetu, Maisha Yetu' ikiwa ina lengo kuu ya kukuza ufahamu, mazungumzo na hatua za mabadiliko juu ya mabadiliko ya hali ya hewa ambayo tayari yamefikiwa kiwango cha dharura kote ulimwenguni.

Kwa upande wake Dulla, ameshukuru uongozi wa tamasha hilo kwa namna ulivyouthamini muziki wa singeli na kueleza kuwa ushiriki wake utamuwezesha kukutana na wasanii wengine wa kimataifa na hivyo kupata uwanda mpana wa kuutangaza muziki huo nje ya nchi.

Naye Meneja wa tamasha hilo, Journey Ramadhani amesema tofauti na miaka mingine ambapo tamasha hilo hufanyika siku nne kwa mwaka huu litafanyika siku mbili yaani Februari 12 hadi Februari 13,2021.

"Kama mnavyojua tamasha lolote linahitaji maandalizi na bajeti katika kulifanya, lakini hakuna asiyejua mwaka jana dunia ilipitia kipindi kigumu cha janga la corona, hivyo hata kupata wadhamini kwa mwaka huu ilikuwa ngumu.

"Ila tulikaa tukatafakari  tukaona kidogo tulichokipata tukitumie hivyohivyo na ndio tukaja na wazo la kupunguza siku na shughuli za kufanya, ambapo sasa hata majukwaa litakuwa moja badala ya matatu" amesema Ramadhani

Balozi wa Norway nchini, Elizabeth Jocobsen amesema tamasha hilo limekuwa likisaidia kwa kiasi kikubwa kutangaza utamaduni wa Mwafrika na kuongeza kuwa utamuduni kwa wasiojua ni haki na Sera ya maenedeleo kwa watu wake hivyo ipo haja ya kuendelezwa nankuenziwa kila iitwapo leo.

Wakati balozi wa Umoja wa Mataifa, Mantredo Fanti amesema muziki kama hiphop, Rock na blues chanzo chake ni muziki wa Afrika na kueleza kuwa kuwa waafrika wana kila sababu ya kujivunia muziki wao na utamaduni wao.

Vikundi vitakavyoshiriki katika tamasha hilo ni pamoja na nchi vinapotoka kwenye mabano, Yugen Black rock (Afrika Kusini), Moreleraba (Lesotho), Djam (Algeria), Sika Kokoo Kokoo (Ghana), Dawda Jobarten (Gambia), SitiMuharam (Zanzibar), Sandra Nankoma (Uganda), Stone Town Rockerz (Zanzibar), Richie Lumambo (Tanzania) na Dogo Fire (Reunion)

Kiingilio katika tamasha hilo kwa watanzania na watu kutoka nchi za Afrika Mashariki kwa siku zote mbili ni Sh10,000 wakati kwa siku moja ni Sh6000.