Ibraah aficha alichoitiwa Basata kuhusu Konde

Muktasari:
- Ibraah amefika ofisi za Basata tangu saa 2:40 asubuhi akiwa ameongozana na mwanasheria wake, ilipofika saa 4 asubuhi aliitwa na mwanasheria wa BASATA, Christopher Kamugisha kwa ajili ya mazungumzo.
Msanii Ibraah aliyeibua mjadala kuhusu kutaka kujitoa Konde Gang ya Harmonize, ameondoka muda huu hapa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), huku akigoma kuzungumza chochote juu ya alichoitiwa.
Ibraah amefika ofisi za Basata tangu saa 2:40 asubuhi akiwa ameongozana na mwanasheria wake, ilipofika saa 4 asubuhi aliitwa na mwanasheria wa BASATA, Christopher Kamugisha kwa ajili ya mazungumzo.
Saa 6 mchana huu, msanii huyo ametoka kwenye chumba cha mwanasheria wa BASATA na kuwaambia wanahabari hawezi kuongea chochote ila wawasiliane na uongozi wa Konde Gang inayomilikiwa na Harmonize.
Hadi ibraah anaondoka Harmonize bado alkuqa hajafika BASATA kuitikia wito uliotolewa jana kutakiwa kuhudhuria kikao hicho saa 2 asubuhi ya leo.
Wasanii hao wamekuwa wakipigana vijembe na kujibizana mtandaoni tangu Ibraah alipotangaza achangiwe Sh 1 Bilioni ili ajitoe Konde Gang.