Jengua afariki Dunia

Muigizaji nguli wa filamu na tamthilia Tanzania, Mohamed Fungafunga maarufu Jengua amefariki dunia asubuhi ya leo, Desemba 15, 202
Taarifa hizo zimethibitishwa na mke marehemu aliyefahamika kwa jina la Maua Ally, amesema Jengua amefariki akiwa Mkuranga, Pwani, nyumbani kwa mtoto wake mkubwa alipokuwa akiuguzwa.
“Alikuwa anasumbuliwa na presha, kwahiyo tulikuwa mkuranga kwa kwa mtoto wake mkubwa kwa ajili ya kumuuguza, lakini leo tumeamka asubuhi hali ikawa mbaya, na akafariki hapa nyumbani,” ameeleza Maua huku akilia

Aidha Maua ameweka wazi kuwa mume wake alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya presha.
Msiba wa mzee Jengua uko Mkuranga nyumbani kwa mwanae, lakini mazishi ya staa huyo yatafanyika Mburahati Dar es Salaam katika makaburi ya Mburahati.

Umaarufu wa Jengua ulianza mwanzoni mwa miaka ya 2000 alipoigiza katika tamthilia ya Kidedea iliyokuwa ikiandaliwa na kikundi cha ChemChem. Kisha baadae alipumzika kuigiza kabla ya kuibuka tena mwaka 2010 na kuanza kuonekana zaidi kwenye filamu.
Imeandikwa na Kelvin Kagambo