Maajabu! Mr Ibu azikwa sebuleni, baada ya siku 118 tangu afariki

Muktasari:

  • Mr Ibu alikumbwa na mauti wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Evercare Likki iliyopo jijini Lagos na tangu wakati huo, mwili wake ulikuwa haujazikwa ikiwa ni takribani miezi minne hadi Ijumaa iliyopita (Juni 28) alipozikwa.

Hatimaye mwili wa mchekeshaji maarufu wa Nigeria, John Okafour 'Mr Ibu' umezikwa majuzi ikiwa ni baada ya kupitia siku 118 tangu alipofariki dunia, Machi 2 mwaka huu.

Mr Ibu alikumbwa na mauti wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Evercare Likki iliyopo jijini Lagos na tangu wakati huo, mwili wake ulikuwa haujazikwa ikiwa ni takribani miezi minne hadi Ijumaa iliyopita (Juni 28) alipozikwa.

Chanzo cha kifo chake kilielezwa ni shambulio la moyo, japo alianza kuugua kiasi cha kukatwa mguu tangu Oktoba mwaka jana. Taarifa zinasema, mchekeshaji huyo mwili wake ulizikwa ndani ya sebule ya nyumba yake iliyopo katika mji aliozaliwa wa Amuri, Jimbo la Enugu ikielezwa na wosia alioutoa enzi za uhai wake.

Hata hivyo, jambo hilo limeelezwa kwa raia wa Nigeria sio kitu cha kushangaza kwa maiti kuzikwa sebuleni au katika eneo jingine la nyumba aliyokuwa akiishi kwani ni moja ya tamaduni zao.

Mazishi yake kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya nchini Nigeria zinaonyesha yamehudhuriwa na wasanii wenzake akiwamo, Patrince Ozonkwor, Angela Okorie na wengine pamoja na ndugu na jamaa zake.

Mr Ibu alianza kuugua Oktoba mwaka jana na mwezi mmoja baadae alifanyiwa upasuaji uliokata mguu wake mmoja kwa kilichoelezwa kuganda kwa damu na hali iliendelea kuwa mbaya kwake akiuguzwa kwa msaada wa wasamaria wema n wasanii wenzake hadi alipokumbwa na mauti.

Enzi za uhai wake, Mr Ibu aliyezaliwa Oktoba 17, 1961 alitaamba na filamu za uchekeshaji na nyingine za kawaida zilizotamba katika ukanda wa filamu wa Nollywood ikihisiwa ameigiza zaidi ya 200 n kabla ya kujitosa kwenye sanaa ya uigizaji alishawahi kuwa Bondia na na kocha wa mpira wa miguu mbalimbali na kuwa karateka.

Katika uhai wake aliwahi kuoa mara mbili na kujaliwa kutapa watoto zaidi ya 10, huku mkewe wa pili akielezwa alizaa naye watoto watatu, huku wa kwanza hafahamiki na baadhi ya kazi zake ni Mr Ibu (2004), Mr Ibu 2 (2005), Mr Ibu and His Son, Coffin Producers, Husband Suppliers, International Players na Store Keeper.

Nyingine ni Issakaba, Mr Ibu in London, Police Recruit, Bafana Bafana, 9 Wives, Ibu in Prisons na Keziah. Pia aliwahi kujitosa kwenye fani ya muziki mwaka 2020 na kutambulisha nyimbo kama 'This Girl' na 'Do You Know'.