Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mama Mobetto afichua mazito baada ya kufanya ‘sajari’

MAMA Pict

Muktasari:

  • Mwonekano mpya wa Mama Mobetto umezua mijadala katika mitandao ya kijamii huku wengine wakihoji kimemkuta kitu gani, lakini mama huyo ameeleza kila kitu wakati alipofanya mahojiano na Mwanaspoti.

Mama Hamisa Mobetto, ambaye jina lake halisi ni Shufaa Lutenga, ameanika ukweli kuhusu mwonekano wake mpya huku akiwapa ujumbe watu wanaomshambulia katika mitandao ya kijamii.

Mwonekano mpya wa Mama Mobetto umezua mijadala katika mitandao ya kijamii huku wengine wakihoji kimemkuta kitu gani, lakini mama huyo ameeleza kila kitu wakati alipofanya mahojiano na Mwanaspoti.

Mama Hamisa muonekano wa umbo lake sasa kuanzia kwenye mabega na kushuka chini limepungua tofauti na zamani alivyozoeleka kuwa na umbo nene, hali iliyozua mijadala kwa kila mmoja kuongea lake, baadhi wakidai huenda anaumwa, au hekaheka za harusi ya mtoto wake, Hamisa alipoolewa na mchezaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki, zimemkondesha.

Akizungumza na Mwanaspoti, mama Mobetto amesema kupungua kwa mwili wake kumetokana na kufanyiwa upasuaji nchini Uturuki kwa ajili ya kupunguza unene ili awe na mwonekano mzuri.

Amesema alikwea pipa kwenda nchini Uturuki kwa ajili ya kufanya upasuaji wa kurekebisha umbo lake hilo na sasa hali yake inaendelea vyema.

Amesema wakati wa harusi ya bintiye alikuwa na maumivu makali kipindi hicho lakini sasa hali yake inaendelea vyema.

Mama Hamisa ameiambia Mwanaspoti kuwa anafurahia alichofanya kwani ni kitu kinachompa furaha ya nafsi siku hadi siku ndiyo maana alitoa pesa kuutengenza mwili wake jinsi anavyopendezwa yeye, japo bado ana maumivu ambayo hayajapona hadi sasa sababu hana muda mrefu tangu afanye upasuaji huo.

"Naona watu wengi wananishangaa mwili wangu kupungua, kila mtu anasema lake, ila hawajui kama mimi nimepunguza mwili kwa kufanya sajari, na hapa kidonda ndio kinapona, kwa sasa mwili nilionao ndiyo naupenda, kwani ule wa mwanzo ulikuwa ukinisababishia presha, miguu kuuma na uvivu wa kufanya jambo mambo mengi.

"Na nimefanya hivi sio sababu ya kufuata mkumbo wa mtu yeyote yule, bali mimi nilitaka kupunguza maradhi madogo madogo yaliyokuwa yananiandama kila uchao, na kufanya hivi sikulazimishwa na mtu yeyote, tatizo watu wengi wanajua ukienda Uturuki au India unakuwa umeenda kwa ajili ya mtu fulani, yaani mtu kamuona mtu kafanya basi naye anaenda, hii kwangu hapana," amesema Mama Hamisa.

"Kwa sasa naendelea vizuri kabisa, na hata maendeleo ya mwili wangu uko poa haswaa, ila nawashangaa watu wanaonishangaa mimi kufanya sajari katika umri huu, sasa sijui wanadhani mimi nimefanya sajari kwa kutaka urembo? Yaani binadamu ni watu wa ajabu sana, au walitaka niliendelee kuteseka na ule mwili wangu wa zamani wa unene sana? Hiki nilichofanya kwa wanaojua madhara ya uzito mkubwa kiafya hawawezi kunishangaa, unene ni hatari. Afya yako ni jukumu lako mwenyewe na sio la watu wengine."

Mwanaspoti lilitaka kufahamu mwanzo alikuwa na uzito wa kilo ngapi na baada ya sajari amefikisha kilo ngapi, mama huyo alisema hiyo ni siri yake.

"Mimi kama nilivyo huwa mambo ya ndani huwa napenda yabaki kuwa siri yangu, ila watu waelewe tu mimi siumwi wala sina stresi zozote, bali nimefanya sajari," amesema.

Kwa sasa kumekuwa na wimbi kubwa la watu nchini kufanya 'sajari' wakiwamo wasanii na watu maarufu katika mitandao ambao wamefanya upasuaji wa kutengeneza baadhi ya viungo vyao vya mwili na wengine wakienda mbali kutaja madhara yaliyowakuta baada ya kufanya hivyo.