Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mama Mobetto bado hajauzoea mwili mpya

MOBETO Pict

Muktasari:

  • Mwonekano huo mpya wa Mama Mobetto umezua mijadala katika mitandao ya kijamii na kila anapoposti picha ama video zake, watu humfananisha na msanii wa Bongo movie, Wema Sepetu ambaye pia alipunguza mwili wake na sasa anaonekana mwembamba.

MAMA Hamisa Mobetto amesema mwili alionao sasa hajauzoea hata kidogo, maana kuna wakati anajisikia mwepesi mpaka anapepesuka.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mama Mobetto alisema ni ngumu kuwa na mwili mnene halafu baadaye kuwa mwembamba, lazima mabadiliko yatokee hasa ukiwa umepunguza kilo nyingi.

“Kiukweli kuna muda nakuwa bado sijauzoea huu mwili hata kidogo, unaweza ukakaa lakini ukiinuka unapepesuka, unajua bado una mwili uleule mkubwa,” alisema Mama Mobetto huku akigoma kusema amepunguza kilo ngapi.

Mama Mobetto hivi karibuni aliliambia Mwanaspoti,kupungua kwa mwili wake kumetokana na kufanyiwa upasuaji nchini Uturuki ili awe na mwonekano mzuri.

Mwonekano huo mpya wa Mama Mobetto umezua mijadala katika mitandao ya kijamii na kila anapoposti picha ama video zake, watu humfananisha na msanii wa Bongo movie, Wema Sepetu ambaye pia alipunguza mwili wake na sasa anaonekana mwembamba.