Mashalove: Sitaki kutumika tena

Muktasari:
- Amesema wanaume wengi wamekuwa hawana msimamo na maisha yake na kuishia kumzeesha jambo ambalo kwa sasa hakubaliani nalo.
MSANII na mrembo wa kwenye video 'Video Vixen', Masha love amesema kwa sasa anajitambua tofauti na miaka ya nyuma na hataki tena kutumika kwa wanaume bila mpango.
Amesema wanaume wengi wamekuwa hawana msimamo na maisha yake na kuishia kumzeesha jambo ambalo kwa sasa hakubaliani nalo.
Akizungumza na Mwanaspoti, Masha love alisema huko nyuma mtu unakuwa na akili ya kitoto hata unapokutana na mtu anakuambia anakupenda na kuamua kuwa naye na baada ya miezi kadhaa mnatengana.
“Sasa hivi jamani nimekua, najitambua vilivyo na uzuri najua yupi anakudanganya au anakupendea umaarufu tu, hivyo mambo ya kutumika bila mpango siku hizi hakuna tena kabisa,” alisema Masha Love
Masha Love kwa sasa yupo kwenye mahusiano na Mose Iyobo, ambaye ni dansa wa msanii Diamond Platnumz.