Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azizi KI agonganisha Waarabu wa Morocco

AZIZ KI Pict

Muktasari:

  • Yanga inapiga hesabu za kumuuza Aziz KI mwisho wa msimu huu, baada ya ofa kubwa tatu lakini mbili kati ya hizo ndio zinaonyesha mwanga mkubwa.

YANGA imekaa mkao wa kuvuna mamilioni ya kufuru kupitia kiungo mshambuliaji, Stephanie Aziz KI lakini huko Uarabuni kuna vita kubwa inapigwa kati ya klabu mbili.

Yanga inapiga hesabu za kumuuza Aziz KI mwisho wa msimu huu, baada ya ofa kubwa tatu lakini mbili kati ya hizo ndio zinaonyesha mwanga mkubwa.

Klabu tatu zinazomtaka Aziz KI zote zinatoka Morocco ambazo ni vigogo Raja Athletic lakini pia kuna Wydad AC na FAR Rabat hao ndio wanapambana kwa nguvu wakipishana kidogo katika ofa zao.

Tuanze na FAR Rabat ambayo ni timu iliyowahi kufundishwa na kocha wa zamani wa Yanga, Nasreddine Nabi, timu hiyo ya jeshi la mfalme imefikia dau linalotakiwa na Yanga na pia hata kwa mchezaji.

Hata hivyo, Wydad baada ya kusikia hivyo, ikamuongezea fedha kidogo mchezaji huyo na wasimamizi wake ili wamshawishi kiungo huyo atue kwao.

Mwanaspoti linafahamu meneja wa kiungo huyo, Zambro Traore, hivi karibuni alikuwa na vikao tofauti na mabosi wa klabu hizo nchini Morocco maalum kwa kusimamia maslahi ya mchezaji huyo.

Ushawishi mkubwa wa Wydad inataka Aziz atue klabuni hapo kuungana na kocha Rulani Mokwena ambaye ni shabiki mkubwa wa kiungo huyo tangu akiwa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Wydad inamshawishi Aziz KI kuachana na ofa zote nyingine ikitaka atue kwao ili akashiriki mashindano mapya ya Klabu Bingwa ya Dunia yatakayofanyika Marekani kati ya Juni na Julai mwaka huu.

Ushawishi huo unaonyesha kuzigawa ofa hizo ambapo Wydad inakaribia kumbadilisha akili Aziz na wasimamizi wake ambao wanaona mashindano hayo yataongeza kitu, lakini shida kubwa ni maslahi makubwa ya Yanga ambayo ndio itatoa jibu la mwisho kukubali ofa ipi kati ya hizo.

“Sisi Yanga tunataka fedha ndefu, unapomuuza mchezaji kama Aziz KI, lazima uelewe kwamba, sio uamuzi rahisi kumuacha mchezaji mwenye kiwango bora kama huyu lakini maslahi pekee ndio yatafanya tukubali,” alisema bosi huyo wa juu wa Yanga.

“Yanga tunataka fedha lakini ushawishi wa Wydad ambao wanataka mchezaji akashiriki mashindano haya mapya ndio yanawagawanya wao kwahiyo acha tuone ni klabu ipi itafanikiwa kukubaliana na pande zote.”

Huu ni msimu wa tatu kwa Aziz Ki tangu aliposajiliwa na Yanga kutoka ASEC Mimosas ya Ivory Coast ambapo ameifungua jumla ya mabao 37 katika Ligi Kuu yakiwamo tisa ya msimu wa kwanza, 21 ya msimu uliopita na saba aliyonayo kwa sasa.