Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Niffer atii agizo la Waziri Mkuu, aripoti Polisi

Muktasari:

  • Majaliwa ametoa amri hiyo jana, Novemba 18, 2024 wakati wa shughuli ya kuaga miili ya watu 15 waliofariki katika ajali hiyo, Majaliwa amekataza watu mitandaoni kuchangisha fedha kwa ajili ya waathirika hao, huku akiliagiza Jeshi la Polisi kumkamata kwa mahojiano ama ajipeleke mwenyewe Kituo cha Polisi.

Wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiliagiza Jeshi la PolisI kumsaka mwanamitandao na mfanyabiashara, Jenifer Jovin 'Niffer' ili kumhoji aliyempa kibali cha kuchangisha rambirambi za waliofariki dunia katika ajali ya ghorofa Kariakoo, mwanamitandao huyo ametii agizo na kuripoti Kituo Kati cha Polisi, Dodoma.

Majaliwa ametoa amri hiyo jana, Novemba 18, 2024 wakati wa shughuli ya kuaga miili ya watu 15 waliofariki katika ajali hiyo, Majaliwa amekataza watu mitandaoni kuchangisha fedha kwa ajili ya waathirika hao, huku akiliagiza Jeshi la Polisi kumkamata kwa mahojiano ama ajipeleke mwenyewe Kituo cha Polisi.

Muda mchache baadae kutoka kwenye akaunti ya Instagram ya mwanamitindo huyo amenukuliwa akisema kuwa: “Nimeitikia wito wa Mhe Waziri na nimekuja kituo cha polisi cha Dodoma. Yote ni miamala mliyoitoa kwa mioyo yenu mizuri kama ambavyo huwa tunafanya mara kwa mara na kwenda kwa watoto Yatima au Kumsaidia yoyote mwenye uhitaji kati yetu.

“Kiwango nilichowatajia ni kilekile na uchunguzi unaendelea.

"Nimechapisha kuanzia mda nilioposti jana mpaka leo wakati nakuja kituoni baada ya kufuta post zote"

Miamala yote ya kampuni ya (akitaja kampuni za simu alizokusanyia fedha hizo) akaweka alama ya kushukuru kisha akamalizia kwa kusema IT WILL ALL BE WELL akimaanisha kila kitu kitakuwa sawa. ASANTENI,”