Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Japan wanapeleka ujuzi wa mbio, chenga Marekani

JAPAN Pict

Muktasari:

  • Lakini unapozungumzia mastaa wakubwa waliowahi kutikisa soka la Japan ni pamoja na Hidetoshi Nakata, aliyeng’ara akiwa na klabu za Italia kama vile AS Roma na Parma, akisaidia kufungua mlango wa wachezaji wa Kijapani kucheza soka la kulipwa Ulaya.

TOKYO, JAPAN: JAPAN ni miongoni mwa mataifa 48 ambayo yatakuwa katika ardhi ya Amerika Kaskazini mwezi ujao kwenye fainali za Kombe la Dunia, likipeleka wakali wake wengi wenye ujuzi wa kuwatoka wapinzani wao kwa kasi sambamba na chenga za maudhi.

Lakini unapozungumzia mastaa wakubwa waliowahi kutikisa soka la Japan ni pamoja na Hidetoshi Nakata, aliyeng’ara akiwa na klabu za Italia kama vile AS Roma na Parma, akisaidia kufungua mlango wa wachezaji wa Kijapani kucheza soka la kulipwa Ulaya.

Pia yupo Shinji Kagawa ambaye alifanya vizuri akiwa na Borussia Dortmund chini ya kocha Jürgen Klopp ambapo alitwaa mataji na kuwa mmoja wa viungo washambuliaji bora Bundesliga. Baadaye fundi huyo alihamia Manchester United na kucheza chini ya Sir Alex Ferguson.

Katika orodha hiyo pia kuna Keisuke Honda, aliyefanya vizuri akiwa na CSKA Moscow na baadaye kuichezea AC Milan.

JAPA 06

Miongoni mwa majina ya kihistoria pia yumo Kazuyoshi Miura ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa soka la kisasa la Japan na bado anakumbukwa kama ishara ya nidhamu na maisha marefu ya soka.

Kutoka kwenye mafanikio ya mastaa hao, Japan imeendelea kukua na kuwa moja ya timu imara barani Asia na duniani huku 2026 ikiwa ni mara yao ya nane kushiriki michuano hiyo ya Kombe la Dunia ambayo hufanyika kila baada ya miaka minne.

Walishiriki fainali za 1998 nchini Ufaransa, kisha 2002 waliposhiriki kama wenyeji pamoja na Korea Kusini, 2006 Ujerumani, 2010 Afrika Kusini, 2014 Brazil, 2018 Russia na 2022 Qatar.

JAPA 01

KABLA YA VITA (1910s–1930)

Timu ya taifa ya Japan ilianza safari yake ya soka la kimataifa katika kipindi cha miaka ya 1910 hadi 1930, kilichojulikana kama 'Pre-war era', kipindi cha kabla ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Mechi za kwanza za kimataifa za Japan zilichezwa 1917 katika 'Far Eastern Championship Games', mashindano ya kimataifa ya michezo yaliyohusisha nchi za Asia ya Mashariki na baadhi ya maeneo ya Asia ya Kusini-Mashariki.

Kwa wakati huo, mashindano hayo yalifanyika Tokyo ambapo Japan iliwakilishwa na timu ya Tokyo Higher Normal School. Ingawa Japan ilifanya vizuri katika michezo mingine kama kuogelea, baseball na riadha, timu yake ya mpira wa miguu ilikumbana na vipigo dhidi ya China na Philippines.

Hata hivyo, mchezo wa soka uliendelea kuenezwa zaidi katika shule za Japan katika miaka ya 1920.

Mwaka 1921 Shirikisho la Soka la Japani lilianzishwa rasmi na mwaka 1929 Japan ikajiunga na FIFA. Hata hivyo, Japan haikushiriki Kombe la Dunia la 1930. Timu ya kwanza ya taifa ya rasmi ilianzishwa mwaka 1930.

Mwaka 1936, chini ya kocha Shigeyoshi Suzuki, Japan ilishiriki kwa mara ya kwanza katika Olimpiki za Berlin, hatua muhimu katika historia ya soka la taifa hilo. Pia Japan ilijiandaa kushiriki kufuzu Kombe la Dunia la 1938 lakini ikajiondoa kabla ya mechi yake dhidi ya Dutch East Indies. Baada ya kuanza kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, shughuli za soka la kimataifa zilipungua na Japan ilicheza mechi chache dhidi ya maeneo yaliyokuwa chini ya utawala wake, ikiwa ni pamoja na Manchuria.

JAPA 02

MAGEUZI YA SOKA

Miaka ya 1990 ilileta mageuzi makubwa katika soka la Japan. Mfumo wa ligi yao, J.League, ulizinduliwa rasmi 1993, hatua iliyobadilisha kabisa taswira ya soka nchini humo na kuongeza ushindani wa ndani.

Mwaka 1992, Japan ilipata mafanikio makubwa kwa kutwaa taji lake la kwanza la AFC Asian Cup baada ya kuifunga Saudi Arabia katika fainali kwa bao 1–0.

Mwaka 1996 Japan ilitetea taji lake la Asian Cup lakini ikatolewa robo fainali, kabla ya kushiriki Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza mwaka 1998 nchini Ufaransa ambapo ilipoteza mechi zote tatu dhidi ya Argentina, Croatia na Jamaica.

JAPA 03

MIAKA YA 2000

Katika miaka ya 2000, Japan ilianza kuonyesha nguvu kubwa ya ushindani kimataifa. Mwaka 2000 ilitwaa tena ubingwa wa Asia na 2002 ilishiriki Kombe la Dunia ikiwa mwenyeji pamoja na Korea Kusini, ikifika hatua ya 16 bora kwa mara ya kwanza.

Mwaka 2004 ilitwaa tena AFC Asian Cup nchini China  na 2006 ilishiriki Kombe la Dunia Ujerumani lakini ikashindwa kufika hatua ya mtoano, 2007 pia ilishindwa kutetea ubingwa wa Asia, ikitolewa nusu fainali na Saudi Arabia.

JAPA 04

MWENDO MDUNDO

Mwaka 2010 ulikuwa wa mafanikio makubwa kwa Japan baada ya kufuzu Kombe la Dunia 2010 kupitia hatua ya mchujo ya Asia na kuwa moja ya timu za kwanza kufika Afrika Kusini.

Katika hatua ya makundi walionyesha ushindani dhidi ya Cameroon, Denmark na Uholanzi, wakifika hatua ya 16 bora kabla ya kutolewa na Paraguay kwa mikwaju ya penalti (5-3) baada ya sare ya 0–0.

Baada ya mashindano hayo, kocha Takeshi Okada alijiuzulu na nafasi yake kuchukuliwa na Alberto Zaccheroni ambaye alileta matokeo chanya mapema kwa kuzifunga timu kama Argentina na Paraguay.

Mwaka 2011 Japan ilishiriki Kombe la Mataifa ya Asia (AFC Asian Cup) na kutwaa ubingwa baada ya kuifunga Australia 1–0.

JAPA 07

Katika safari ya kuelekea Kombe la Dunia 2014, Japan ilicheza kwa kiwango kizuri na kufuzu kwa urahisi lakini kwenye mashindano yenyewe walishindwa kuvuka hatua ya makundi baada ya kufungwa 2–1 na Ivory Coast, sare ya 0–0 dhidi ya Ugiriki na kufungwa 4–1 na Colombia.

Mwaka 2015 Japan ilianza vizuri kwenye AFC Asian Cup kwa kushinda mechi zote za makundi bila kuruhusu bao lakini ilitolewa katika robo fainali na UAE. Matokeo haya yalikuwa pigo kubwa na kusababisha mabadiliko ya benchi la ufundi ambapo Vahid Halilhodzic alichukua nafasi ya ukocha.

Chini ya Halilhodzic ambaye aliwahi kuinoa Raja Casablanca ya Morocco, Japan ilipitia kampeni ngumu ya kufuzu Kombe la Dunia 2018 lakini hatimaye walifanikiwa baada ya kuifunga Australia 2–0.

Hii ilihakikisha kushiriki kwao kwa mara ya sita mfululizo kwenye mashindano ya dunia.

Kombe la Dunia 2018 lilikuwa la kihistoria kwa Japan baada ya kuifunga Colombia 2–1, ikiwa ni ushindi wa kwanza kwa timu ya Asia dhidi ya timu ya Amerika Kusini kwenye mashindano rasmi ya FIFA.

Walifuzu hatua ya 16 bora kwa faida ya kadi za nidhamu (fair play), lakini walitolewa na Ubelgiji baada ya kupoteza uongozi wa mabao 2–0 na kufungwa 3–2.

Mwaka 2019 Japan ilifika fainali ya AFC Asian Cup lakini ikafungwa na Qatar 3–1. Pia walishiriki Copa America ambapo walitoa changamoto lakini hawakufuzu hatua ya mtoano.

Katika Kombe la Dunia 2022, Japan ilifanya maajabu kwa kuifunga Ujerumani kwa mabao 2-1 na Hispania kwa mabao 2-1 na kufuzu hatua ya 16 bora kama vinara wa kundi E. Hata hivyo walitolewa na Croatia kwa penalti 3-1 baada ya kutoka sare ya bao 1-1.

Kufikia miaka ya 2020 na kuelekea 2026, Japan iliendelea kuwa nguvu kubwa, ikishinda mashindano ya EAFF 2022 na kufuzu mapema Kombe la Dunia 2026. Waliongeza rekodi kwa kuifunga England katika mchezo wa kirafiki kwa bao 1–0 Wembley mwaka 2026, ushindi ulioweka historia kama moja ya matokeo makubwa zaidi ya soka la Asia dhidi ya Ulaya.

JAPA 05

MASTAA WAO

Takefusa Kubo ni mmoja wa wachezaji muhimu wa kizazi kipya cha Japan ambaye kwa sasa anachezea Real Sociedad nchini Hispania.

Kubo mwenye mabao mawili na asisti nne katika La Liga amejijengea jina kutokana na uwezo wake mkubwa wa kumiliki mpira, kupiga chenga za haraka na kutengeneza za mabao.

Akiwa mchezaji wa kiungo mshambuliaji au pembeni, mara nyingi ndiye anayebeba mzigo wa ubunifu kwenye safu ya ushambuliaji ya Japan.

Kaoru Mitoma ni winga hatari anayekipiga katika Brighton & Hove Albion kwenye Ligi Kuu England, anacheza ligi moja na nahodha wake wa timu ya taifa, Wataru Endo (Liverpool).