Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kuelekea Kombe la Dunia, mastaa Madrid watemwa Hispania

SPAIN Pict
SPAIN Pict

Muktasari:

  • Ripoti zinasema kuwa, kiwango na uwezo wa kujituma kwa wachezaji wazawa wa Real Madrid msimu huu ulikuwa chini sana. Hali hii imemlazimu kocha De la Fuente kufanya uamuzi magumu na kuwatema kuelekea fainali hizo zitakazopigwa nchini Marekani, Canada na Mexico.

KOCHA Mkuu wa Hispania, Luis de la Fuente, ametangaza kikosi kwa ajili ya kushiriki Fainali za Kombe la Dunia 2026, huku akileta mshangao mkubwa baada ya kuwaacha wachezaji wa Real Madrid. Hii ni tofauti kabisa na miaka ya nyuma ambapo nyota wa Madrid walikuwa nguzo kwenye timu ya taifa hilo.

Ripoti zinasema kuwa, kiwango na uwezo wa kujituma kwa wachezaji wazawa wa Real Madrid msimu huu ulikuwa chini sana. Hali hii imemlazimu kocha De la Fuente kufanya uamuzi magumu na kuwatema kuelekea fainali hizo zitakazopigwa nchini Marekani, Canada na Mexico.

Kikosi cha Hispania kilichotangazwa kinaundwa na makipa Unai Simón (Athletic Club), David Raya (Arsenal) na Joan García (Barcelona).

Mabeki; Marc Cucurella (Chelsea), Alejandro Grimaldo (Bayer Leverkusen), Pau Cubarsí (Barcelona), Aymeric Laporte (Athletic Club), Marc Pubill (Atlético Madrid), Eric García (Barcelona), Marcos Llorente (Atlético Madrid) na Pedro Porro (Tottenham).

Viungo; Pedri (Barcelona), Fabián Ruiz (PSG), Martín Zubimendi (Arsenal), Gavi (Barcelona), Rodri (Manchester City), Álex Baena (Atlético Madrid) na Mikel Merino (Arsenal).

Washambuliaji; Mikel Oyarzabal (Real Sociedad), Dani Olmo (Barcelona), Nico Williams (Athletic Club), Yéremy Pino (Crystal Palace), Ferran Torres (Barcelona), Borja Iglesias (Celta Vigo), Víctor Muñoz (Osasuna) na Lamine Yamal (Barcelona).