Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Darassa, Harmonize wanaendelea walipoishia!

VIBE Pict

Muktasari:

  • Mapema wiki hii Darassa ameachia wimbo wake mpya, Love Design (2026) akimshirkisha Harmonize, ambao umetayarisha na Abbah huku video yake ikiongozwa na Bless Dollar.

RAPA kutokea Classic Music Group (CMG), Darassa kwa mara nyingine tena ameshirikiana na mwimbaji wa Bongofleva, Harmonize ambaye ni mwanzilishi wa Konde Music Worldwide.

Mapema wiki hii Darassa ameachia wimbo wake mpya, Love Design (2026) akimshirkisha Harmonize, ambao umetayarisha na Abbah huku video yake ikiongozwa na Bless Dollar.

Ikumbukwe hatua hiyo imekuja ikiwa ni takribani miezi mitatu tangu Darassa alipoachia kolabo yake na mwanamuziki wa Hip Hop kutokea Kenya, Khaligraph Jones ambaye amesikika katika ngoma, Beginning (2026).

Kwa mara ya kwanza wawili hao kufanya kazi pamoja, ni pale Darassa alipomshirikisha Harmonize katika wimbo wake, Yumba (2019), kisha Mazoea (2024), na sasa Love Design (2026).

VIB 02

Hii inamfanya Harmonize kuwa miongoni mwa waimbaji wa Bongofleva waliofanya kolobo nyingi zaidi na Darassa baada ya Ben Pol, Marioo na Alikiba kutokea Kings Music.

Kwa upande wake Harmonize, amemshirikisha Darassa katika remix ya wimbo wake ‘Bedroom’ kutoka katika albamu yake ya kwanza, Afro East (2020).

Mbali na Darassa, remix hiyo iliwakutanisha wasanii wengine wengi ambao ni Country Wizzy, Young Lunya, Salmin Swaggz, Moni Centrozone, Billnass, Rosa Ree, Baghdad na Nay wa Mitego.

VIB 04

Ushirikiano kati ya Darassa na Harmonize, ni mwendelezo wa rapa huyo kufanya kazi na waimbaji wenye nguvu kubwa ya ushawishi, kitu ambacho kimepelekea kupata namba kubwa kwenye majukwaa ya kidijitali.

Kwa sasa Darassa ndiye rapa namba moja Bongo katika majukwaa yote ya kusikiliza muziki mtandaoni ikiwemo YouTube Music, Spotify, Boomplay, Apple Music n.k.

Vilevile ndiye mwanamuziki wa kwanza wa rap Bongo kufanikiwa kufikisha wafuasi (subscribers) milioni 1 katika mtandao wa YouTube ambao alijiunge nao mnamo Novemba 2015.

VIB 07

Mafanikio hayo yamekuja kutokana na namna ambavyo amefanikiwa kubadili mtindo wa muziki wake na kuja kivingine kwa lengo la kulishika zaidi soko la muziki.

Waimbaji wengine waliosikika katika ngoma za Darassa ni Rich Mavoko, Maua Sama, Jux, Nandy, Mbosso na Zuchu. Vilevile kuna Bien kutokea Kenya, na Sho Madjozi wa Afrika Kusini.

Hivyo si ajabu kuona video za nyimbo zake zote ambazo zimetazamwa zaidi ya mara milioni 10 katika mtandao wa YouTube ni zile alizoshirikiana na wasanii wengine, yaani kolabo.

VIB 03

Wasanii hao ni Ben Pol (Muziki), Harmonize (Mazoea), Sho Madjozi (I Like It), Mbosso (Looking For You), Alikiba (Proud of You), Nandy & Marioo (Loyalty) na Bien (Nobody). 

Utakumbuka Darassa alitoka rasmi kimuziki kupitia wimbo wake, Sikati Tamaa (2012) akimshirikisha Ben Pol, kolabo iliyotayarishwa na Bob Manecky katika studio za AM Records.

Baadaye sana alikuja kufanya kolabo nyingine na Ben Pol, Muziki (2016) ambayo sasa inashikilia rekodi kama video ya msanii wa rap Bongo iliyofanya vizuri zaidi YouTube ikitazamwa (views) mara milioni 36.

VIB 05

Mwaka uliopita, Darassa alitamba na kolabo yake na Mbosso ‘Looking For Love’, na ndio wimbo uliopokelewa vizuri zaidi kutokea katika albamu yake ya pili, Take Away The Pain (2025) iliyotoka chini ya CMG ikiwa na nyimbo 15.

Wimbo huo uliotayarishwa na Kaniba, video yake ilitoka Februari 14 chini ya Mjukuu Visuals, na tayari imetazamwa mara milioni 22 huko YouTube, na ilishika nafasi ya sita katika orodha ya video za Bongofleva zilizofanya vizuri zaidi 2025.

Miongoni mwa wasanii wengine walioshirikishwa katika albamu hiyo ni Alikiba, Zuchu na Jay Melody huku wa kimataifa wakiwa ni wawili pekee ambao ni Bien na Jovial, wote wakitokea Kenya.

VIB 06

Hiyo inamfanya Alikiba kuwa mwanamuziki pekee ambaye amesikika katika albamu zote mbili za Darassa ambazo ni Slave Becomes a King (2020) na Take Away The Pain (2025).

Ikumbukwe albamu ya kwanza ya Darassa ilitoa nyimbo nyingi maarufu, moja wapo ni Loyalty (2020) akiwashirikisha wadogo zake kimuziki, Nandy na Marioo.

Ulifanya vizuri na kumpatia tuzo yake ya kwanza ya muziki Tanzania (TMA) ambapo ulishinda kama Wimbo Bora wa Kushirikiana 2021 baada kuzibwaga nyimbo kama Ndombolo (Alikiba), Shikilia (Professor Jay), Unaua Vibe (Rapcha) na Lala (Jux).

Huo ulikuwa ni wimbo wa pili kwa Darassa kumshirikisha Marioo baada ya ule wa Chanda Chema (2019) uliomrudisha vizuri katika muziki baada ya ukimya mrefu wa tangu Agosti 2017 hadi Septemba 2018, kwa kile alichodai alikuwa kwenye mapumziko.