Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Matukio maarufu mastaa kuvutwa nywele uwanjani

NYWELE Pict

Muktasari:

  • Kadi nyekundu ya Lisandro Martinez kumvuta nywele Calvert-Lewin iliigharimu Man United Jumatatu ilipochapwa mabao 2-1 na mahasimu wao hao wakubwa katika Uwanja wa Old Trafford.

LONDON, ENGLAND: KATIKA soka kuna matukio mengi ambayo huwaacha vinywa wazi mashabiki na hata wachezaji wenyewe, ambayo hufanyika kinyume na sheria au kanuni za mchezo huo, huku yakilazimisha mamlaka husika kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wahusika.

Hivi ulishawahi kusikia kwamba kunamatukio ya ndani ya uwanja, lakini yaliishia wachezaji kufungwa gereni?  Mwaka 2004 James Cotterill aliyekuwa akiichezea Bournemouth alifungwa jela miezi minne England kwa kosa la kumvunja taya mchezaji wa Bury wakati wa mchezo wa FA na Joey Barton 2008 alikamatwa na kufungwa miezi sita kwa kosa la vurugu nje ya uwanja baada ya mechi wakati akiichezea Man City.

Lakini, kuna matukio mengine yanaishia uwanjani ingawa ni mashambulizi dhidi ya mwili ambayo mamlaka za soka zimeamua adhabu zake ziishie ndani ya dimba kama kupigana viwiko, kukwatuana makusudi na kuvunjana mifupa, kupigana hadharani na kadhalika.

Na katika siku za karibuni ulimwengu wa soka umekumbushwa tena juu ya matukio ya wachezaji wa soka kushikana nywele katika matukio ya kugombea mpira uwanjani na wiki iliyopita lilikuwa ni tukio ambalo liliadhibiwa kwa kadi nyekundu ambayo baadaye iliibua utata dhidi ya Lisandro Martinez wa Manchester United aliyeonekana aking’ang’ania nywele za straika wa Leed United, Dominic Calvert-Lewin.

Kadi nyekundu ya Lisandro Martinez kumvuta nywele Calvert-Lewin iliigharimu Man United Jumatatu ilipochapwa mabao 2-1 na mahasimu wao hao wakubwa katika Uwanja wa Old Trafford.

Ingawa kuvuta nywele hakutajwi moja kwa moja katika sheria za mchezo, kitendo hicho hutafsiriwa kama utovu wa nidhamu wa kutumia nguvu bila kujali nia au ukubwa wake, jambo ambalo mara nyingi husababisha mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki, wachezaji na makocha kuhusu kadi nyekundu zinazoonekana kuwa 'laini' uwanjani.

Kadi hiyo ilitolewa baada ya mwamuzi wa VAR, John Brooks, kumtaka mwamuzi wa kati, Paul Tierney, kurejea kwenye kioo kupitia upya tukio la kuvutwa nywele kwa Calvert-Lewin. Kufuatia kadi hiyo, Lisandro Martinez sasa anatarajiwa kukosa mechi tatu, huku kocha wa muda wa Manchester United, Michael Carrick, akishindwa kuficha hasira zake. Carrick ameuita uamuzi huo kuwa ni wa 'kushangaza' na 'mbaya zaidi' kuwahi kushuhudiwa uwanjani msimu huu

Tangu kuanzishwa kwa VAR, kadi nyekundu kwa makosa ya aina hiyo zimekuwa za kawaida zaidi. Mapema mwaka huu, beki wa Everton Michael Keane alitolewa uwanjani kwa kumvuta nywele mshambuliaji wa Wolves, Tolu Arokodare, na kupewa adhabu ya kukosa mechi tatu, jambo lililomkera kocha wa Everton, David Moyes. Ingawa siku hizi wachezaji wanaadhibiwa mara kwa mara zaidi, matukio ya kuvutwa nywele yamekuwepo katika soka kwa muda mrefu. Haya hapa ni baadhi ya matukio maarufu yaliyowahi kuzua mjadala kwa miaka mbalimbali.

NYWE 05

CRISTIANO ROMERO DHIDI YA MARC CUCURELLA

Nyota wa Chelsea, Cucurella, aliwashambulia kwa maneno makali viongozi wa waamuzi wa Chama cha Waamuzi wa Soka England (PGMOL), baada ya beki wa Tottenham Hotspur, Romero, kuepuka adhabu kufuatia tukio la kumvuta nywele Agosti 2022.

Mchezo kati ya Spurs na Chelsea katika Uwanja wa Stamford Bridge uligeuka kuwa wa vurugu baada ya Cucurella kuvutwa chini nywele zake wakati Romero akijaribu kushambulia mpira wa kona, ambapo mwamuzi Anthony Taylor na mwamuzi wa VAR, Mike Dean waliamua kutomchukulia hatua beki huyo baada ya kupitia tukio hilo.  Spurs waliendelea na mechi na kulazimisha sare ya mabao 2-2 kupitia bao la dakika za mwisho la Harry Kane, jambo lililosababisha ugomvi kati ya makocha Antonio Conte na Thomas Tuchel baada ya mechi.

Romero hakuadhibiwa wakati wa mchezo wala hakuchukuliwa hatua baadaye, licha ya Cucurella kusisitiza kwa hasira kuwa kulikuwa na kosa, huku Mike Dean baadaye akikiri kufanya makosa.

NYWE 04

MAROUANE FELLAINI DHIDI YA MATTEO GUENDOUZI

Aliyekuwa kiungo wa Manchester United, Fellaini, alizua mjadala baada ya kumvuta nywele kiungo wa Arsenal, Guendouzi, katika sare ya 2-2 mwaka 2018. Mbelgiji huyo alimrudisha nyuma Guendouzi kwa kumvuta nywele zake ndefu, akimtupa chini ili kuzuia shambulizi hatari la Arsenal. Cha kushangaza, hakupata hata kadi ya njano kutoka kwa mwamuzi Andre Marriner, licha ya mechi hiyo ya Ligi Kuu England kuwa kali na kuonyesha kadi sita za njano.

NYWE 03

PETER CROUCH DHIDI YA BRENT SANCHO

Mshambuliaji wa zamani wa England, Crouch, aligeuka kuwa adui namba moja nchini Trinidad & Tobago katika fainali za Kombe la Dunia 2006  baada ya kutumia nywele za Sancho kujisaidia kufunga bao. Kwa kuvuta nywele za beki huyo, Crouch alipanda juu na kufunga bao muhimu lililovunja ukimya kabla ya Steven Gerrard kufunga la pili dakika ya 90 na kuifanya England kushinda 2-0. Sancho aliliita tukio hilo “shambulio la kimwili† katika mahojiano, akidai mwamuzi alimpuuza waziwazi.

NYWE 02

JACK STEPHENS DHIDI YA MARC CUCURELLA

Tukio jingine la kuvutwa nywele lililomhusisha Cucurella lilitokea Desemba 2024, safari hii mchezaji alichukuliwa hatua. Beki wa Southampton, Stephens, alitolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumvuta nywele nyota huyo ndani ya eneo la penalti.

Mwamuzi Tony Harrington alipewa ushauri na VAR kupitia tukio hilo na akaamua kutoa kadi nyekundu kwa kosa la kutumia nguvu. Chelsea waliibuka na ushindi wa mabao 5-1, huku Cole Palmer na Jadon Sancho wakifunga mabao baada ya Southampton kubaki na wachezaji 10.

NYWE 01

ROBERT HUTH DHIDI YA MAROUANE FELLAINI

Mei 2016, Fellaini alivutwa nywele na beki wa Leicester City, Huth, katika tukio lililosababisha wote wawili kufungiwa mechi tatu baadaye.

Wakati wakipambana kuwania mpira, Huth alimvuta nywele Fellaini ambaye naye alijibu kwa kumpiga kiwiko usoni. Tukio hilo halikuonwa na waamuzi uwanjani, lakini lilipitiwa baadaye na jopo la waamuzi wa zamani waliothibitisha kuwa wote walistahili adhabu.

Akimtetea Fellaini baada ya mechi, kocha wa wakati huo wa Manchester United, Louis van Gaal, alisema: “Haipo kwenye sheria kwamba mtu anatakiwa kushikwa nywele na kuvutwa nyuma. Hiyo ipo tu kwenye mambo ya masoko ya ngono.