Harry Maguire aongezewa adhabu England
Muktasari:
- Beki huyo wa England, 33, alitolewa kwa kadi nyekundu katika mechi dhidi ya Bournemouth mwezi uliopita na tayari hadi sasa ameshakosa mechi moja.
MANCHESTER, ENGLAND: CHAMA cha soka cha England, kimethibitisha Harry Maguire ataukosa mchezo wa Manchester United dhidi ya Chelsea baada ya kuongezewa adhabu ya kufungiwa mechi moja zaidi.
Beki huyo wa England, 33, alitolewa kwa kadi nyekundu katika mechi dhidi ya Bournemouth mwezi uliopita na tayari hadi sasa ameshakosa mechi moja.
Hata hivyo, pia ataukosa mchezo wa Jumamosi dhidi ya Chelsea utakaochezwa Stamford Bridge kutokana na adhabu hiyo ya iliyosababishwa na utovu wa nidhamu.
Jumatano, FA ilitangaza baada ya kikao huru cha kusikiliza shauri hilo, shtaka hilo limethibitishwa na Maguire amepewa adhabu ya kufungiwa mechi moja zaidi na faini ya Pauni 30,000.
Beki huyo alishtakiwa kwa kitendo chake alichokifanya baada ya kutolewa dakika ya 78 katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Bournemouth uliochezwa Ijumaa Machi 20.
Ilidaiwa kuwa Maguire alitenda alitumia maneno ya matusi au ya kukera kwa mwamuzi wa mezani baada ya kutolewa uwanjani.
Katika maelezo ya adhabu hiyo, ilidaiwa alimwambia mwamuzi wa nne: “Ninyi wote mnafanya utani tu,” alipokuwa anatoka uwanjani. Hata hivyo, Maguire alipinga madai hayo akisema alimaanisha hali ya tukio hilo ilikuwa ya “utani,” si kumtukana mwamuzi.
Pamoja na utetezi wake, kikao hicho kilikubaliana na ripoti ya mwamuzi.
Kukosekana kwa Maguire ni pigo kwa Kocha Michael Carrick, ambaye pia ataikosa huduma ya Lisandro Martinez aliyepata kadi nyekundu dhidi ya Leeds.
Hali hiyo inawapa nafasi mabeki vijana Leny Yoro na Ayden Heaven kuanza katika mechi hiyo muhimu dhidi ya Chelsea.
Mancr United inapanga kukata rufaa kupinga kadi nyekundu aliyopewa Martinez baada ya kumvuta nywele Dominic Calvert-Lewin, wakidai hakutumia nguvu kubwa katika tukio hilo alilofanya wakati akigombea mpira.