Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maguire akalia kuti kavu, asubiri hukumu

MAGUERE Pict

Muktasari:

  • Nahodha wa timu, Bruno Fernandes pia alionyesha hasira, akisema uamuzi huo haukuwa wa haki, akilalamikia kutokuwepo kwa usawa katika maamuzi ya VAR.

MANCHESTER,  ENGLAND: BEKI wa Manchester United, Harry Maguire ameitwa kwenye kamati ya nidhamu ya Chama cha Soka cha England kujibu mashtaka kutokana na jinsi alivyoonyesha utovu wa nidhamu baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika mechi iliyomalizika kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Bournemouth.

Maguire, mwenye umri wa miaka 33, alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya 78 katika mechi hiyo ya Ligi Kuu England baada ya kumuangusha mshambuliaji wa Bournemouth, Evanilson, ndani ya eneo la penalti.

Uamuzi wa refa Stuart Attwell uliungwa mkono na VAR, na Bournemouth ilipata penalti iliyotokana na tukio hilo.

Maguire alikasirishwa na uamuzi huo na akamfuata refa pamoja na mwamuzi wa mezani, Matt Donohue, hali iliyopelekea kuingia matatani.

Taarifa ya FA ilisema: “Harry Maguire amefunguliwa mashtaka baada ya kutolewa kadi nyekundu katika dakika ya 78 ya mechi ya Manchester United dhidi ya Bournemouth. Inadaiwa kuwa alitumia maneno au vitendo visivyofaa, vya matusi au vya kudhalilisha dhidi ya mwamuzi wa mezani baada ya kutolewa kwake.

Maguire alitakiwa kwenda kujibu tuhuma hizo hadi kufikia Aprili 2, kisha kusubiria hukumu ambayo itatolewa.

Mbali na kesi hiyo, kwa sasa Maguire tayari amepewa adhabu ya kukosa mechi moja, hivyo hatocheza dhidi ya Leeds United Aprili 13, lakini adhabu hiyo inaweza kuongezwa kutokana na mashtaka mapya. Mechi inayofuata ya United baada ya Leeds ni dhidi ya Chelsea ugenini Aprili 18, na hiyo pia kuna uwezekano asicheze.

Kocha wa muda wa Man United, Michael Carrick, hakuridhishwa na kadi nyekundu hiyo, akisema timu yake ilipaswa kupewa penalti mapema katika mechi hiyo baada ya Adrien Truffert kumfanyia madhambi Amad Diallo.

Nahodha wa timu, Bruno Fernandes pia alionyesha hasira, akisema uamuzi huo haukuwa wa haki, akilalamikia kutokuwepo kwa usawa katika maamuzi ya VAR.