Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Meja Jenerali Isamuhyo hapana kipengele

MEJA Pict

Muktasari:

  • Sasa macho, masikio na hisia zetu hapa kijiweni tunaelekeza katika dabi ya pili ya Kariakoo ambayo itapigwa keshokutwa tu hapo Jumapili  ikiwa ni siku nne tu tangu dabi ya juzi.

JUZI dabi ya kwanza ya Kariakoo imemalizika kule Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar na mnyama Simba kaibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga.

Sasa macho, masikio na hisia zetu hapa kijiweni tunaelekeza katika dabi ya pili ya Kariakoo ambayo itapigwa keshokutwa tu hapo Jumapili  ikiwa ni siku nne tu tangu dabi ya juzi.

Ile ya juzi ilikuwa Kariakoo Dabi ya Kombe la Muungano na sasa inakwenda kupigwa ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya NBC ambayo itafanyika katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo kule Mbweni Dar es Salaam.

Baada ya Simba kutangaza kuwa mchezo huo ambao wao watakuwa ni wenyeji, tumeona maoni tofauti yakitolewa ambapo baadhi wanaonekana kuikosoa Simba kwa kuchagua Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo kwa kucheza mechi hiyo.

Eti wanaamini kwa Simba kuchagua uwanja huo, inaishusha hadhi Kariakoo Dabi na badala yake wanadhani ilipaswa ichague uwanja mwingine ambao unaingiza idadi kubwa ya mashabiki kama CCM Kirumba Mwanza.

Hii ni hoja ambayo haina mashiko kwa vile Dabi ya Kariakoo ukubwa na uzito wa thamani yake hauwezi kushushwa kwa sababu ya uwanja au uchache wa mashabiki kwani huo hizo timu mbili zimekuwa kubwa kwa sababu nyingi zaidi hata ya idadi ya mashabiki wa kuingia uwanjani kwenye mechi baina yao.

Pia Kijiwe kinaamini jambo la kwanza na la msingi katika soka ni lile eneo ambalo wachezaji wanalitumia katika dakika 90, ndio linatakiwa kuwa bora zaidi kuliko hata hayo mambo ya mashabiki kwa vile bila hilo huo mpira wenyewe utapoteza ladha.

Sasa Uwanja wa Meja Isamuhyo ni miongoni mwa viwanja vichache sana hapa nchini ambavyo vina eneo bora la kuchezea lenye nyasi za asili zinazotunzwa vyema kila siku iendayo kwa Mungu.

Pia pale kuna usalama wa kutosha na hakuna hayo mambo sijui ya kulinda uwanja hivyo aliye bora atashinda vizuri tu hakuna makandokando pale.