Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

PANGA: Kikosi cha Real Madrid kufanyiwa mabadiliko

PANGA Pict

Muktasari:

  • Katika klabu inayojulikana kwa ubora wake wa makocha, nafasi ya kocha Alvaro Arbeloa iko hatarini. Mara ya mwisho Real Madrid ilimaliza misimu miwili mfululizo bila taji kubwa ilikuwa 2009-10, ambapo iligeukia enzi mpya chini ya Jose Mourinho.

MADRID, HISPANIA: BAADA ya kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Bayern Munich wiki iliyopita, tathmini ya ndani ya kikosi hicho imeshaanza kuelekea mwisho wa msimu ambao huenda ikaumaliza bila kombe lolote.

Wakati timu hiyo ikiwa nyuma ya Barcelona kwa idadi kubwa ya pointi katika Ligi Kuu Hispani (La Liga), zikiwa zimesalia mechi sita, inaonekana kuwa kwa msimu wa pili mfululizo timu haitabeba taji kubwa.

Katika klabu inayojulikana kwa ubora wake wa makocha, nafasi ya kocha Alvaro Arbeloa iko hatarini. Mara ya mwisho Real Madrid ilimaliza misimu miwili mfululizo bila taji kubwa ilikuwa 2009-10, ambapo iligeukia enzi mpya chini ya Jose Mourinho.

PANG 03

Safari hii mashabiki wanaweza kuona mabadiliko kadhaa muhimu yakifanyika nje ya benchi la ufundi pia na kuna sababu nzuri ya kuangalia zaidi ya kocha, kwani Carlo Ancelotti aliondoka Mei, mwaka jana, Xabi Alonso alifutwa kazi Januari, mwaka huu na sasa Arbeloa naye anaonekana kuondoka. Ikiwa wote hao wameonekana kushindwa ni kawaida sasa macho kuelekezwa kwa wachezaji.

Kutoridhika kwa mashabiki kwa baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza tayari kumesikika katika Uwanja wa Bernabeu msimu huu. Kylian Mbappe, Jude Bellingham na Vinicius Junior wote wamewahi kuzomewa na kupigiwa miluzi na mashabiki nyumbani mara kadhaa tangu Alonso afutwe kazi. Pia kumekuwapo na wito kwa rais Florentino Perez kujiuzulu.

The Athletic imepitia kikosi cha Real Madrid na kuonyesha maeneo gani yanayoweza kubadilika na kwa nini. Taarifa hizi zinatokana na mazungumzo na vyanzo mbalimbali vilivyo karibu na klabu ambavyo vilizungumza kwa siri kulinda mahusiano.

PANG 02

MAKIPA

Hii ndiyo nafasi yenye mjadala mdogo zaidi kutokana na ubora wa Thibaut Courtois na Andriy Lunin. Hakuna mipango ya haraka ya kubadilisha eneo la makipa.

Courtois atatimiza umri wa miaka 34 mwezi Mei, mwaka huu akiwa na mkataba unaoendelea hadi 2027, na amekuwa mchezaji thabiti zaidi msimu huu. Jeraha la paja alilopata dhidi ya Manchester City, Machi 17, lilikuwa pigo kubwa, na alikosekana katika kipigo cha robo fainali dhidi ya Bayern Munich.

Ubora wa Lunin katika mechi zote mbili dhidi ya mabingwa hao wa Ujerumani umekosolewa. Ingawa alifanya uokoaji muhimu, pia alihusika katika kosa lililosababisha bao la kwanza la Bayern Munich.

Mchezaji huyo wa Ukraine mwenye umri wa miaka 27 ameonyesha kujitoa katika nafasi yake ya kuwa chaguo la pili nyuma ya Courtois, na ana mkataba hadi 2030. Hata hivyo, baadhi ya watu waliomzunguka wanashauri aangalie uwezekano wa kuondoka ili kupata muda zaidi wa kucheza.

Iwapo ataondoka, Real Madrid italazimika kuamua kama itampandisha kipa wa timu ya vijana, Fran Gonzalez, au kuingia sokoni kutafuta mwenye uzoefu zaidi.

PANG 06

MABEKI

The Athletic iliripoti Februari kulikuwa na mashaka juu ya kuongeza mkataba wa nahodha Dani Carvajal, unaoisha Juni. Kutokuwepo kwa maendeleo na muda mdogo wa kucheza kwa Carvajal kunaashiria kuwa hakuna ofa itakayotolewa.

Mchezaji mwenyewe pia amekuwa na mashaka, na sasa akiwa na umri wa miaka 34, alitaka kuon geza mkataba kama angekuwa fiti na akiwa na nafasi muhimu. Anadaiwa kufadhaika kwamba hapati nafasi zaidi ya kuthibitisha ubora wake uwanjani.

Carvajal alijiunga na akademia ya Real Madrid 2002 na amekuwa klabuni hapo tangu wakati huo, isipokuwa msimu mmoja tu alipokwenda Bayer Leverkusen 2012-13. Kuondoka kwake kutaiacha Real Madrid na Trent Alexander-Arnold pekee kama beki wa kulia.

Kwa mabeki wa kati, mkataba wa David Alaba unaisha na hatapewa mpya. Eder Militao, 28, na Antonio Rüdiger, 33, wote wamekuwa wakipata majeraha ya mara kwa mara. Mkataba wa Rudiger pia unaisha msimu huu wa joto na klabu inashughulikia suala hilo. Militao ana mkataba hadi 2028.

Mhitimu wa akademi ya Real Madrid, Raul Asencio, 23, alipandishwa timu ya kwanza wakati wa tatizo la majeraha ya mara kwa mara ya wachezaji wenzzake 2024 na akasaini mkataba mpya hadi 2031, ambao bado haujatangazwa rasmi. Anaonekana kuwa mchezaji anaye weza kuuzwa.

Dean Huijsen, 21, hachezi kila wiki na amekuwa na matatizo ya majeraha msimu huu, lakini bado anaonekana kuwa mchezaji muhimu wa muda mrefu baada ya kusajiliwa kwa Pauni 50 milioni 50 kutoka Bournemouth majira ya joto ya msimu uliopita. Ingawa Real Madrid huenda ikahitaji angalau usajili wa mastaa wawili zaidi katika eneo la ulinzi wa kati, hali ya beki wa kushoto siyo ya haraka kiasi hicho.

Alvaro Carreras alijiunga msimu uliopita wa kiangazi kwa Euro 50 milioni kutoka Benfica na ana mkataba hadi 2031. Ferland Mendy amekuwa na matatizo ya majeraha msimu huu, lakini hufanya vizuri pale anapohitajika na amesifiwa na Arbeloa na mashabiki. Kulingana na vyanzo vya klabu, mkataba aliouo ngeza 2024 unaendelea hadi 2027. Wakala wake anadai unaendelea hadi 2028.

Fr an Garc ía amefungwa mkataba hadi 2027, ingawa alipata nafasi ya kuondoka kwenda Bournemouth, Januari, lakini Real Madrid ilizuia uhamisho huo. Mustakabali wake kikosini unaweza kufanyiwa mapitio mwisho wa msimu, lakini hakuna dalili za mazungumzo ya kuongeza mkataba.

PANG 04

VIUNGO

Hii ni nafasi nyingine muhimu inayohitaji kuimarishwa, kwani kuondoka kwa Luka Modric na Toni Kroos kuliacha pengo kubwa, hasa kwa mchezaji wa kudhibiti tempo ya mchezo. Eduardo Camavinga yupo katika hali ya kutathminiwa upya, na ingawa ameonyesha nia ya kubaki, lakini kiwango chake kimekuwa cha kusuasua. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa anaonekana kukosa umakini katika mechi muhimu.

Licha ya ubora wake katika nyakati fulani, anaonekana kuwa na tatizo la kupoteza umakini katika mechi muhimu. Sasa akiwa na umri wa miaka 23, alijiunga kutoka Rennes mwaka 2021 na bado hajajithibitisha kikamilifu. Anaweza kuwa mchezaji wa kuuzwa ikiwa ofa nzuri itatoka Ligi Kuu ya England. Mkataba wake unaisha 2029.

Kama ilivyoripotiwa awali na The Athletic, Dani Ceballos anataka kuondoka. Hali hiyo imekuwepo katika masoko kadhaa kutokana na muda mdogo wa kucheza na nia ya kurudi Real Betis. Mkataba wake unaisha 2027, na anatarajiwa kuondoka msimu huu wa joto.

Kuondoka kwa viungo wengine kutakuwa mshangao. Aurelien Tchouaméni, Arda Güler, Federico Valverde na Bellingham wanaonekana kuwa nguzo za muda mrefu za klabu hiyo. Lakini kuna sintofahamu kuhusu Franco Mastantuono.

Mastantuono ana umri wa miaka 18, lakini usajili wake wa Euro 63.2 milioni ulikuwa ghali zaidi kwa Real Madrid msimu uliopita wa kiangazi. Katika msimu, amepoteza nafasi kikosini. Hata hivyo, upande wake unadai hakuna mipango ya kuondoka na unataja mfano wa Guler ambaye pia alihitaji muda ili kuanza kupata namba. Swali ni kama atapata muda huo Real Madrid ikiwa usajili mpya utafanyika. Kwa majina ya kuangaliwa katika usajili wa kuingia, Nico Paz ndiye muhimu zaidi. Real Madrid ina kipengele cha kumnunua tena nyota huyo wa Argentina mwenye miaka 21 ambaye amevutia akiwa Como katika Ligi Kuu Italia (Serie A) pamoja na Jacobo Ramon, beki wa kati mwenye miaka 21 na mhitimu mwingine wa akademia ya Madrid.

Kwa upande wa Dani Ceballos naye anatarajiwa kuondoka kutokana na kukosa nafasi na nia yake ni kurejea Real Betis. Wachezaji kama Aurelien Tchouameni, Federico Valverde, Arda Guler na Jude Bellingham wanaonekana kuwa msingi wa muda mrefu wa kikosi hicho huenda wakabaki, lakini miongoni mwao wanaweza kuchomolewa na kuuzwa katika timu zingine Ulaya.

PANG 01

WASHAMBULIAJI

Kuna haja ya kuongeza nguvu katika eneo hili ambayo siyo kubwa sana, lakini mabadiliko bado yanaweza kutokea na ni wazi yanahitajika kwa haraka. Vinicius Junior na Kylian Mbappe bado hawajapata muunganiko mzuri wa kiwango cha juu ule wa mara kwa mara. Mara nyingi mmoja hucheza vizuri wakati mwingine hayupo sahihi kivile.

Pia kumekuwapo na ukosoaji kuhusu juhudi zao wanapokosa mpira, hasa kwa Mbappe anayeonekana anatembea tu uwanjani bila kupambana kutafuta mpira au kuonyesha juhudi za kuwasaidia wenzake kuuweka miguuni mwao, hivyo anapaswa kuangaliwa kwa jicho la karibu au kumtafutia mtu atakayeelewana naye.

Mkataba wa Vinicius Jr unaisha mwishoni mwa msimu ujao, lakini alishasema katika mkutano na waandishi wa habari Aprili 6 kwamba anataka kubaki klabuni “kwa miaka mingi†. Mazungumzo ya mkataba mpya yalisimama mwaka jana. Vipindi ambapo wote wawili wamekuwa katika viwango bora kwa pamoja ni vichache. Mara nyingi, nyakati hizo zimekuja wakati mmoja kati yao akiwa hayupo.

Katika nafasi ya mshambuliaji wa kati, Arbeloa hajamtegemea sana Gonzalo García, aliyekuwa mfungaji bora kwenye Kombe la Dunia la Klabu msimu uliopita na vyanzo vya karibu na nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 vinadai machaguo mengi yalikuwa mezani kwake kutoka klabu mbalimbali tangu dirisha la Januari, mwaka huu.

Kwa upande mwingine, Rodrygo Goes atakuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na jeraha kubwa la goti, hivyo hatauzwa kwa sasa, lakini mara tu ataporejea atapaswa kupambana kurejesha kiwango alichokuwa nacho wakati anasajiliwa.

Upande wa Endrick anatarajiwa kurejea kutoka kwenye mkopo katika Klabu ya Lyon ya Ufaransa, ambako hata hivyo kiwango chake hakijaonekana kuwa cha juu kama ilivyotarajiwa. Nyota huyo wa Kibrazili alipopelekwa Lyon kwa mkopo ilitarajiwa kwamba angefanya zaidi kuliko alipokuwa kikosini Madrid. Timu hiyo pia imekosa mshambuliaji mwenye nguvu na uzoefu tangu kuondoka kwa Joselu, aina ya mchezaji wa kuingia dakika za mwisho kubadili matokeo, hivyo italazimika kuingia sokoni kupata mtu wa aina hiyo. Kwa jumla, Real Madrid wanakabiliwa na kipindi muhimu cha kufanya uamuzi mgumu.

Ingawa makocha wamekuwa wakilaumiwa, lakini macho yanaelekezwa kwa kikosi chenyewe. Mabadiliko makubwa yanaonekana kuwa njiani, si tu kwenye benchi la ufundi bali pia ndani ya kikosi chenyewe.